ANGALIA HAPA JINSI RAISI WA ATLETICO ALIVYOWAKATA MAINI MAN U NA REAL MADRID - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, November 18

ANGALIA HAPA JINSI RAISI WA ATLETICO ALIVYOWAKATA MAINI MAN U NA REAL MADRID

RAIS wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo amedai kuwa hakuna nafasi kwa mshambuliaji wao Antoine Griezmann kujiunga na Real Madrid au Manchester United.

Image result for griezmann
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa jina lake limehusishwa na vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya katika miezi ya karibuni kufuatia kuimarika kwa kiwango chake.

Tetesi za kuhamia Old Trafford nazo zilizuka huku Griezmann akikiri kuwa angefurahi kucheza sambamba na Mfaransa mwezake Paul Pogba huku Madrid nao wakitajwa katika mbio za kumuwania.

Hata hivyo, tetesi hizo zimezimwa na Cerezo akidai kuwa haamini kama mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ataweza kwenda Madrid au klabu nyingine yeyote ile.

Cerezo aliendelea kudai kuwa wamekuwa na uhusiano mzuri na Madrid na wanaheshimiana kama majirani.

 Atletico wanatarajiwa kuikaribisha Madrid katika mchezo wa La Liga kesho, ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana toka Atletico walipofungwa katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa matuta Mei mwaka huu kule San Siro.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here