MTU MREFU ZAIDI TANZANIA KUPATA HUDUMA INDIA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, November 18

MTU MREFU ZAIDI TANZANIA KUPATA HUDUMA INDIA

Zahanati  nchini India imejitolea kumsaidia mwanamme kutoka nchini Tanzania, ambaye aliambiwa kuwa kutokana na urefu wake, hawezi kufanyiwa upasuaji nchini Tanzania.
Baraka Elias akiwa amesimama na mwandishi wa BBC Lizzy Masinga
Daktari katika zahanati ya Speedy Recovery, ameiambia BBC kuwa wanaweza kumsaidia Baraka Elias, ambaye madaktari mjini Dar es Salaam wanasema hawezi kutoshea katika kitanda cha hospitali.
Elias aliye na urefu wa futi 7.4 au mita 2.20, anasema anahitaji kufanyiwa upasuaji baada ya kuumia alipoanguka.
Pia aliambiwa kuwa hangeweza kutoshea kwa mashine ya X-ray kutokana na urefu wake.
"Nina uhakika kuwa bwana Elias atapata nafuu hivi karibuni, wakati akifahamu kuwa kuna mtu mbali sana anajaribu kumfanyia maabo kuwa sawa," Dr Shaila Raveendran anayeongoza zahanati ya Speed Recovery nchini India, 
Bwana Elias anatajwa kuwa mtu mrefu zaidi nchini Tanzania.
Source:BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here