WAGANGA WA ASILI WAWALALAMIKIA WALE WANAOPIGA LAMLI KUSABABISHA MAUAJI YA ALBINO - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, November 17

WAGANGA WA ASILI WAWALALAMIKIA WALE WANAOPIGA LAMLI KUSABABISHA MAUAJI YA ALBINO

NA ANAEL JAMES WAZIRITALL

Umoja wa waganga wa tiba  asiliaa (UWAWATA) wamesisitiza kwa wanachama kukamilisha michango yao waliyo ahidi katika kituo cha kulea watu wenye ulemavu wa ngozi Albino.

Hayo yamesemwa katika kikao mbele ya mratibu wa mratibu wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa shinyanga bwn LAZARO ANAEL wakati akiongea na waganga hao na kuomba  kuaminika kuwa sio waganga wote wanahusika na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi  yaani Albino na kusisitiza kusakwa kwa waganga wanaopiga ramli chonganishi.

Lakini mbali na hapo Mratibu wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa shinyanga wakati akiongea na mimi katika kikao hicho aliweza kuwaelimisha waganga wa tiba asilia juu ya watu wenye ualbino na kusema kuwa wote wapo sawa na inatakiwa kuondoa matabaka yaliyopo ili uwepo usawa na pia waweze kusaidia jamii katika kupinga waganga wapiga kamli chonganishi ili na wao waweze kuishi kwa kuwa wana haki ya kuishi

Lakini pia Katibu wa nidhamu kanda ya ziwa na mjumbe wa kamati ya nidhamu kitaifa BWN DAVID SIMLEMBE amewataka waganga wa tiba asili kujitambua kwa mambo wanayoyafanya na pia  kutimiza ahadi waliyo ahidi katika kituo cha watu wenye ulemavu wa ngozi albino na kuwaomba waganga wote kukutana katika kikao cha jumamosi ili kuzungumzia mambo mengi yanayowakabili.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here