MAVUGO:SITAKI MANENO NASUBIRI TAREHE MOJA. - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, September 26

MAVUGO:SITAKI MANENO NASUBIRI TAREHE MOJA.

Na Anael James Waziri_Tall

Ni kauli ya Staa huyo wa Wekundu wa msimbazi Wakati zikiwa zimebaki siku nne pekee kabla ya mechi ya watani Simba na Yanga kupigwa, mshambuliaji wa huyo, Mrundi, Laudit Mavugo, ameweka bayana yeye haongei  sana kuhusu mchezo huo utakavyokuwa, lakini anasubiri tu siku ifike ili aonyeshe makali yake uwanjani.



Mshambuliaji huyo  aliyeifungia Simba mabao matatu mpaka sasa, kwa mara ya kwanza anatarajia kuiongoza timu yake hiyo kuvaana na Yanga katika mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Oktoba Mosi, mwaka huu.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Vital’O ya Burundi, amesema licha ya presha ya mchezo huo inavyozidi kupanda lakini kwa upande wake hataki kuzungumzia lolote kuhusiana na wapinzani wao, bali atawaonyesha watakapokutana uwanjani.

“Mechi itakavyokuwa vyovyote kwangu sawa kwa sababu nipo tayari na nimejiandaa kucheza na sina wasiwasi ila kwa wale ambao watataka kuona nitafanya nini basi waje kuona uwanjani na siyo kuanza kuongea sana kabla mechi yenyewe haijachezwa,” alisema mshambuliaji huyo wa Wekundu wa msimbazi .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here