YANGA WAJIPANGA UPYA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, September 26

YANGA WAJIPANGA UPYA

Na Anael James Waziri_Tall
 
Baada ya kuchezea kichapo cha  bao 1-0 kutoka kwa wapiga debe wa Stendi ya Shinyanga, Stand United Chama la wana, Kikosi cha Yanga kinatarajia kuendelea kuweka kambi kanda ya ziwa, kwa ajili ya kujiandaa na mechi yake dhidi ya watani wao wa jadi, Simba itakayochezwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.



Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, alisema kikosi chao kinatarajia kuendelea kuweka kambi katika kanda ya ziwa kabla ya kurejea kwa ajili ya kuwakabili wekundu wa msimbazi Simba Oktoba Mosi.

“Kikosi chetu kitaendelea kuweka kambi katika kanda ya ziwa  kwa ajili ya kujiandaa na mechi yetu dhidi ya Simba ambapo tutarejea siku chache kabla ya mchezo huo.

“Mchezo dhidi ya Simba ni wa kawaida kwetu na tunajiandaa kama ilivyo kwa mechi nyingine kwani tumeshakutana na timu kubwa na kuonyesha uwezo mkubwa Zaidi, hivyo tunaupa uzito sawa mchezo huo na ile mingine na kikubwa Zaidi mwalimu hajatoa ripoti ya mchezaji yoyote aliye majeruhi,” alisema katibu huyo wa wana Jangwani Baraka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here