LIVERPOOL NA ARSENAL WAO WAFUZU ROBO FAINALI KAZI LEO NI KWA MANCHESTER DARBY - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, October 26

LIVERPOOL NA ARSENAL WAO WAFUZU ROBO FAINALI KAZI LEO NI KWA MANCHESTER DARBY

NA ANAEL JAMES WAZIRITALL
Klabu ya Liverpool wao wamefanikiwa kuwabwaga Tottenham 2-1 katiika Mechi ya Raundi ya 4 ya EFL CUP ambalo ndio Kombe la Ligi huko England katika Mechi iliyochezwa Uwanjani Anfield hapo Jana na kutinga moja kwa moja  Robo Fainali.

Magoli ya Liverpool yote yalifungwa na Daniel Sturridge katika Dakika za 9 na 64 na lile la Tottenham kuingizwa Dakika ya 76 kwa Penati ya Janssen.
Kwa upande wao washika mtutu wa jiji la London, Arsenal nao wameingia Robo Fainali baada ya kuipiga Reading Bao 2-0 zote zikifungwa na Alex Oxlade-Chamberlain.
Hull City, wakicheza Ugenini, wameingia Robo Fainali kwa mara ya pili mfululizo Jana walipoitoa Bristol City 2-1 na kwa Bao za Harry Maguire na Michael Dawson huku Bristol wakifunga Bao lao kupitia kwa Tomlin.
Newcastle wametinga Robo Fainali kwa kishindo kwa kuinyuka Preston Northen 6-0 kwenye Mechi iliyochezwa Saint James Park na Wafungaji Bao hizo ni Aleksandar Mitrovic, Bao 2, Mohammed Diame, Bao 2, Matt Ritchie, kwa Penati, na Ayoze Perez.
Mechi kati ya Leeds United na Norwich City ilipigwa Dakika 90 na kuwa Sare 1-1 na kisha zikaenda Dakika za Nyongeza 30 na kuwa 2-2 na mwisho Mikwaju ya Penati Tano Tano ikaipa Leeds ushindi wa Penati 3-2.
Kazi iliobaki ni kati ya mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa soka dunani ni ule wa Manchester United dhidi ya Man City mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Old Trafford leo hii Jumatano.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here