SIMBA WAFATA POINTI SITA MBEYA KWA HASIRA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, October 6

SIMBA WAFATA POINTI SITA MBEYA KWA HASIRA

NA ANAEL JAMES WAZIRITALL
 
Simba SC imejipanga vilivyo kuelekea Mkoani Mbeya kucheza mechi zake mbili ikiwemo ya Wagonga Nyundo wa Jiji la Mbeya (Mbeya City) na ile ya Majeshi yaGereza (Tanzania Prisons).
 
 
Japo kikosi hicho kilipanga  kuondoka mapema jijini Dar es Salaam ili ipate nafasi ya kucheza mechi moja ya kirafiki mkoani Iringa hali imebadilika na kushindikana kuwa hivyo kama ilivyobainishwa na Meneja wa Timu hiyo ya Msimbazi Mussa Mgosi.

Kikosi cha Simba ndiyo kipo kileleni mwa Ligi Kuu Bara kikiwa kina jumla ya pointi 17 na ni mechi za mwanzo nje ya jiji la Dar Es Salaam.

Mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya Mbeya City Jumatano ijayo mjini Mbeya.

Tayari Kocha Mkuu, Joseph Omog ameeleza kwamba kuna mambo kadhaa ya kubadilisha.

Omog amesema kuna mambo ya kubadilisha kwa kuwa viwanja vya mikoani ni tatizo kubwa na lazima kuwe na mbinu tofauti kiuchezaji.

Katika mechi saba zilizopita, Simba imeshinda tano na kutoka sare mbili hivyo kuifanya iendelee kukaa kileleni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here