WAGOMBEA WA TUZO YA BALLON D"OR HADHARANI - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, October 24

WAGOMBEA WA TUZO YA BALLON D"OR HADHARANI

NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL

MAJINA ya Wagombea 30 wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2016, Ballon d'Or, yameanza kutangazwa Leo kwa kutolewa Majina Matano ya mwanzo.


Majina hayo yatakuwa yakitangazwa hii Leo kwa Mafungu ya Majina Matano Matano kila baada ya Saa 2 na ya kwanza kurushwa ni yale ya Sergio Aguero (Manchester City), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund), Gareth Bale (Real Madrid), Gianluigi Buffon (Juventus) na Cristiano Ronaldo (Real Madrid).

Safari hii Tuzo hii imerudi tena kwenye usimamizi wa Jarida la huko Nchini France, France Football, ambao ndio Waasisi wa Ballon d'Or tangu Mwaka 1956 baada ya FIFA kujitoa ushiriki wake.

FIFA waliungana na France Football Miaka 6 iliyopita na kuibatiza Tuzo hii FIFA Ballon d'Or.

Mshindi wa Mwaka Jana alikuwa Lionel Messi mbae ameitwaa Tuzo hii mara 5 ikiwa ni Rekodi.
Mara ya mwisho kwa Tuzo hii kutwaliwa na Mchezaji ambae si Messi wala Cristiano Ronaldo ni Mwaka 2007 wakati Mbrazil Kaka, aliekuwa akiichezea AC Milan ya Italy, kuitwaa.

Mwaka Jana Wachezaji Watano waliokuwa wakicheza Ligi Kuu England waliteuliwa kwenye Listi ya awali ya Wachezaji 23 na hao ni Watatu wa Manchester City, Yaya Toure, Sergio Aguero na Kevin de Bruyne, pamoja na wa Arsenal Alexis Sanchez na wa Chelsea Eden Hazard.

Wengine waliokuwemo humo na sasa wapo Ligi Kuu England ni Wachezaji wa Manchester United Paul Pogba, aliekuwa Juventus, na Zlatan Ibrahimovic, aliekuwa Paris St-Germain.

Kawaida Listi hii ya awali hupunguzwa hadi Wachezaji Watatu ambao hutinga Fainali na kuchaguliwa Mshindi kati yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here