NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta hatashiriki kambi ya wiki moja ya timu hiyo nchini Misri, na badala yake atajiunga na wenzake Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Lesotho.
Taifa Stars watamenyana na Lesotho Juni 10, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Meneja wa Taifa Stars, Danny Msangi ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Samatta hataiwahi kambi ya Misri kwa sababu anakabiliwa na majukumu katika klabu yake, KRC Genk nchini Ubelgiji.
Msangi amesema kwamba, kiungo Farid Malik Mussa atajiunga na timu nchini Misri akitokea Hispania anakochezea DC Tenerife ya Daraja la Kwanza, ingawa bado anakomazwa kikosi cha pili.

No comments:
Post a Comment