wa mawasiliano katika ikulu ya White House amejiuzulu miezi mitatu pekee baada yake kupewa kazi hiyo na Rais Donald Trump.
Mike Dubke, ambaye ni mwanamikakati wa chama cha Republican aliyebobea, alipewa kazi mwezi Machi kujaribu kufanyia mageuzi mkakati wa mawasiliano wa ikulu hiyo.
Kama sehemu ya mabadiliko aliyopendekeza, afisa wa habari wa White House Sean Spicer ataendelea kushikilia wadhifa wake, lakini vikao vya maafisa hao na wanahabari vitakuwa vichache.
Mabadiliko hayo yametokea huku kukiwa na taarifa kwamba kuna migawanyiko katika kundi la maafisa wa mawasiliano White House.
Bw Dubke ameondoka kwa nia njema, kwa mujibu wa tovuti ya kisiasa ya Axios News ambayo ilikuwa ya kwanza kutangaza habari hizo.
Mshauri wa White House Kellyanne Conway amesema Bw Dubke alikuwa amekubali kusalia kazini hadi Bw Trump arejee kutoka safari yake ya kwanza nje ya nchi hiyo Mashariki ya Kati na Ulaya siku ya Jumamosi.
"Ameeleza nia yake ya kutaka kuondoka White House na kusema wazi kwamba atasubiri hadi rais amalize ziara yake ya kimataifa," aliambia Fox News.
Rais Trump anadaiwa kukatishwa tamaa na taarifa zinazotolewa na White House pamoja na uchunguzi wa wabunge na FBI kuhusu iwapo maafisa wake wa kampeni walishirikiana na maafisa wa Urusi kumsaidia kushinda urais.
Majuzi, alitoa wazo la kufutilia mbali vikao vya kila siku vya kuwapasha habari waandishi na badala yake kuwa akiandaa vikao hivyo mara moja kila baada ya wiki mbili.
No comments:
Post a Comment