Upepo mkali unatarajia kuvuma Pwani - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, May 30

Upepo mkali unatarajia kuvuma Pwani


Wanaotumia bahari wametakiwa kuchukua tahadhari Tanzania

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa tahadhari ya kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya pwani ya Tanzania.

Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mamlaka hiyo, kupitia taarifa, imesema kunatarjiwa kuwepo na upepo mkali wa kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayozidi mita 2.

"Msukumo wa upepo wa Kusi unatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda wa pwani ya Tanzania," mamlaka hiyo ilisema.

"Watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari na hatua stahiki."
upepo mkali kuvuma Pwani ya
Hali hiyo ya hewa inatarajiwa kuwepo hadi kufikia kesho 31 Mei.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here