Kesi ya Agnes Masogange yapelekwa mbele - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, July 13

Kesi ya Agnes Masogange yapelekwa mbele


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu imekwama kusikiliza kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili video Queen, Agnes Gerald 'Masogange' kwa sababu ana tatizo la kiafya.

Hayo yameelezwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya wakili wa serikali, Costantine Kakula kueleza shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Hata hivyo, wakili wa Masogane, Ruben Simwanza alimueleza Hakimu kwamba mteja wake anaumwa hivyo anaomba kesi iahirishwe.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 25, 2017 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here