Mayweather na McGregor kutupiana cheche - MKWELITZ BLOG

.

demo-image-Recovered

.

Capture

Thursday, July 13

Mayweather na McGregor kutupiana cheche


_96917885_mayweathermcgregor_rex3
Floyd Mayweather na mpinzani wake Conor McGregor waliendelea kurushiana cheche za maneno katika siku ya pili ya kampeni ya kuuza pigano lao mnamo mwezi Agosti mjini Las Vegas.

Aliyekuwa bingwa wa dunia mara tano katika zni wa middleweight Myweather alikutana tena na bingwa wa uzani wa lightweight mpiganaji McGregor.

McGregor mwenye umri wa miaka 28 alicheza densi katika jukwaa akimkosoa Mayweather mwenye umri wa miaka 40.

Wawili hao watakutana katika piogano lka raudni 12 chini ya sheria za ndondi tarehe 26 mwezi Agosti.

Katika msururu wa kushushaiana matusi Nyota mpiganaji McGregor alimtusi kuhusu nguo aliovaa na hata kusema kuwa hawezi kusoma.

Nakaaje? McGregor aliuuliza umati, kabla ya kulekeza kidole chake kwa begi aliyobeba Mayweather.

Ana miaka 40! Vaa kama umri wako, sio kubeba begi la shule katika jukwaa.

Unafanaya nini na begi la shule katika jukwaa? Huwezi hata kusoma.

Mayweather aliyevalia Tisheti na kofia huk McGregor akiwa amevalia suti, alijibu.Ni mimi ambaye siwezi kusoma? Nafanya hesabu, na natengeza fedha
Unadaiw fedha, McGregor alimjibu, akizungumza kutoka na ripoti kwamba Mayweather aliitaka IRS mapema mwezi huu kupewa muda zaidi wa kulipa kodi ya mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad