AUBEMAYANG KUHAMIA REAL MADRID - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, November 25

AUBEMAYANG KUHAMIA REAL MADRID


Image result for aubameyang

Star wa Borussia Dortmund mara nyingi amehusishwa na story za kutaka kujiunga na club ya Real Madrid. Aubameyang ambae anaendelea kuonyesha kiwango kwa kufunga magoli 15 kwenye mechi 16 msimu huu amesema kwamba hana uwezo wa kuzuia tetesi zozote zinazojitokeza kuhusu yeye.
Alipoulizwa kuhusu kuhamia Real Madrid alionekana kwamba uwezekano huo upo na kuna watu wake wa karibu watakua na furaha kama atahamia hapo,“Mungu pekee ndio anajua nini kitatokea kwenye siku zijazo.Kama likija swala la kujiunga huko(Real Madrid) basi babu yangu atakuwa na anajivunia sana mimi. Babu yangu ametokea kwenye mji mdogo pembeni kidogo ya Madrid.”
Kauli yake inaonyesha kwamba swala la Aubemayang kuhamia Real Madrid halitakua swala la bahati mbaya. Kuhusu mkataba wake alisema hivi,“Nimesaini mkataba na BVB sio kwa bahati mbaya, tetesi zote zinazotokea kwenye habari siwezi kuzizuia. Nime sign mkataba wa muda mrefu na Borussia Dortmund hadi 2020”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here