CRISTIAN RONALDO NA BENZEMA KUKOSEKANA MADRID WIKI HII,HABARI KAMILI NA MKWELITZ BLOG. - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, December 9

CRISTIAN RONALDO NA BENZEMA KUKOSEKANA MADRID WIKI HII,HABARI KAMILI NA MKWELITZ BLOG.


Image result for RONALDO


Cristiano Ronaldo na Kari
m Benzema hawamo kwenye Kikosi cha Real Madrid ambacho Jumamosi kinacheza Mechi ya La Liga na Deportivo La Coruna Uwanjani Santiago Bernabeu Jijini Madrid huko Nchini Spain.



Kwa vile nae Gareth Bale ni Majeruhi, basi Real, ambao wanaongoza La Liga wakiwa Pointi 6 mbele ya Mabingwa FC Barcelona, itakuwa imekosa Fowadi yake yote kamili ya Timu ya Kwanza.

Pia, Kocha Zinedine Zidane ameamua kumpumzisha Kiungo mahiri Luka Modric kwa ajili ya Mechi hii.
Image result for BENZEMA
Real haijafungwa katika Mechi 34 mfululizo na hii wameifikia Rekodi ya Klabu hiyo iliyowekwa huko nyuma!Zidane ameamua kumchukua Fowadi wa Timu yao ya Rizevu, Mariano, ili aungane na Alvaro Morata na Lucas Vazquez kwenye Mashambulizi kwa ajili ya Mechi hii na Deportivo ambao wako Nafasi ya 16 kwenye La Liga wakiwa Pointi 21 nyuma ya Vinara Real.
Zidane hakusema kwa nini Mastaa wake wako nje lakini Real, baada ya Mechi hii, wanasafiri kwenda Japan kucheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu wao wakiwa ndio Wawakilishi wa Bara la Ulaya baada ya kutwaa Kombe la UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here