
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo mapema leo
amefunga bao lake la 500 kwa klabu katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi
ya Club America kwenye michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia.
Ronaldo mwenye umri
wa miaka 31, alifunga bao lake la 500 kwa klabu na nchi yake katika mchezo
dhidi ya Malmo Septemba mwaka jana na sasa amefikisha bao la 500 kwa klabu
pekee.
Nyota huyo alifunga bao hilo katika dakika 90 ya mchezo akiwahadaa walinzi
wa America lakini ilibidi asubiri mwamuzi Enrique Caceres wa Venezuela kwenda
kuangalia upya kama alikuwa kaotea kupitia mfumo mpya wa picha za video wa VAR
unaotumika kwenye michuano hiyo.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye
alijiunga na Madrid kwa ada iliyovunja rekodi mwaka 2009, amefunga bao lake la
500 katika mechi 689 pekee alizocheza.
Ronaldo alifunga bao lake la 377 katika
mechi 367 na pia alifunga mabao 118 katika mechi 292 alizoichezea Manchester
United na matano katika mechi 31 alizocheza Sporting Lisbon.
No comments:
Post a Comment