SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF
kesho linatarajia kufanya sherehe ya kutoa tuzo kwa wachezaji mbalimbali wa
soka waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka mzima uliopita.
Sherehe hizo zinakuwa ni za 25 toka
kuanzishwa kwake na zinatarajiwa kufanyika jijini Abuja, Nigeria kwa mara ya
pili mfululizo.
Kwenye sherehe hizo atapatikana
mfalme wa soka Afrika ambapo miongoni mwao ni pamoja na mshindi wa tuzo ya
mwaka jana Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Riyad Mahrez wa Algeria na Sadio
Mane anayetoka Senegal.
Kuanzia mwaka 1992 zilipoanzishwa
tuzo hizo ambapo ilikwenda kwa nguli wa zamani wa Ghana Abeid Ayew Pele mpaka
mwaka jana alipotwaa Aubameyang ni jumla ya wachezaji 15 waliofanikiwa kutwaa
hiyo.
Nyota wa Cameroon Samuel Eto’o ndio
mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mara nne mfululizo mwaka 2003, 2004, 2005
na 2010 kabla ya Yaya Toure wa Ivory Coast hajaivunja rekodi hiyo kwa kutwaa
kuanzia mwaka 2011 mpaka 2014.
No comments:
Post a Comment