Jafo: ufisadi,wizi unatokana na kutokuwa na imani ya mungu - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, June 4

Jafo: ufisadi,wizi unatokana na kutokuwa na imani ya mungu


Wazazi kote nchini na ulimwenguni kwa ujumla wametakiwa kuwapeleka watoto wao katika taasisi za dini ili kujifunza elimu yakumjua mola wao kwani ndio njia pekee yakuwainua watoto katika misingi ya kuitambua dini yao na kuwa na maadili mazuri

Akiongea katika mashindano yakusoma navkuhifadhi Qur'an tukufu yaliyoandaliwa na taasisi ya kiislamu ya Aswhabulkahfi iliyopo yombo katika wilaya ya temeke jijini Dar es salaam mbunge Naibu Waziri wa Tamisemi na mbunge wa kisarawe muheshimiwa Suleiman jafo amewaomba viongozi wa dini na na wazazi kushirikiana ilibkuwainua vijana katika maadili mema.

Jafo ameongeza kuwa serikali inakumbwa na matatizo ya ufisadi na uwizi kutokana na kukosekana kwa kwa kutomtambua na kuwa na imani ya mola wao

Kwa  upande mkuu wa wilaya ya kinondoni muheshimiwa Ali Hapi amesema kuwa ili kupata viongozi bora na wenye kumcha mungu ni lazima wazazi wajitahidi katika kuwasomesha elimu ya kumtambua mola wao

Aidha Hapi ameahidi kushirikiana na waislamu katika jambo lolote atakalohitajika huku akisistiza kuwa umoja ni jambo la  muhimu miongoni mwa waislamu na wanajamii kwa ujumla.

Taasisi ya Aswhabulkahfi huandaa mashindano ya qura n kila mwaka ifikapo mwezi wa ramadhani kama njia moja wapo yakuwatia motisha wanafunzi wanahofadhi kitabu kitukufu cha Qur'an

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here