Rais Mugabe ameanza kampeni hizo akionekana kuwavutia vijana.
Hapo Ijumaa rais Mugabe alianza kampeni zake kwa kutembelea eneo la Marondea , eneo ambalo linapatikana katika umbali wa kilomita 80 na jiji la Harare.
Katika eneo hilo rais Mugabe alifanya kampeni katika uwanja wa Rudhaka .
Licha ya kutuhumiwa kudhoofisha sekta ya kilimo baada ya kuwanyanganya wakuliwa wa kizungu mashamba, rais Mugabe amesema kuwa uchumi wa Zimbabwe unafanyiwa njama na Magharibi.
Rais Mugabe aliendelea kusema kuwa Zimbabwe sio taafa maskini na kuahidi kuwa katika sekta ya kilimo mavuno yataongezeka katika zoa la mahindi na tumbaku.
Mugabe atakuwa atakuwa mgombea wa kiti cha urais kupitia chama ZANU –PF katika uchaguzi unaotarajiwa katikati mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment