Wakisomewa mashitaka hayo katika Mahakama ya Wilaya Tarime katika kesi ya jinai namba 108/2017 jana mbele ya Hakimu Mkazi Marther Mpaze, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Bukuru Bugombe alidai washitakiwa kwa pamoja Julai 13, mwaka huu mchana katika Mtaa wa Nkende, Tarafa ya Inchage, washitakiwa Omahe, Onchiri na Wanjoi walimshambulia kwa mapanga Mnuve katika ugomvi ambao alikatwa mkono wa kulia na sikio na kusababisha madhara makubwa na ulemavu wa kudumu.
Washitakiwa hao walikana mashitaka hayo na upande wa mashitaka ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Bukuru alipinga dhamana kwa washitakiwa hao na kupelekwa mahabusu hadi Agosti 3, mwaka huu wakati kesi yao itakapotajwa tena.
Katika kesi zingine mbili za jinai zenye namba 109/2017 na nyingine ya mauaji yenye namba 437/2017 zinazowakabili washitakiwa wawili ukiacha mwanamke huyo, ni kupatikana na mali za wizi katika nyumba walimokuwa wakiishi zikiwemo laptop, simu za mkononi, mkanda wa jeshi, visu, mapanga na makofia ya kuficha uso.
Kesi nyingine ni mauaji ya mkazi wa Nkende, Nyaulan Isack aliyedaiwa kuuawa Novemba 3, 2016, na wote walikana mashitaka hayo yote matatu na kupelekwa mahabusu.



No comments:
Post a Comment