Ajali ya treni yaua watu 23 India - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, August 20

Ajali ya treni yaua watu 23 India


Watu takriban 23 wameripotiwa kufariki na wengine 81 kujeruhiwa vibaya baada ya treni kuacha mkondo wake Kaskazini mwa India.

Kwa mujibu wa habari,tukio hilo limetokea katika mji wa Khautali kilomita 100 kutoka mji mkuu wa New Delhi.

Treni hiyo ilikuwa ikitokea mji wa Puri kuelekea mji wa Haridwar.

Waziri wa uchukuzi  Suresh Prabhu ametaka uchunguzi wa makini ufanyike kufuatia ajali hiyo na kusema kuwa hatua muhimu zitachukuliwa.

Hata hivyo mpaka sasa haijajulikana ni nini hasa kimesababisha treni hiyo kuicha njia ya reli ghafla.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here