Ibrahimovic akaribia kurudi Man United - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, August 22

Ibrahimovic akaribia kurudi Man United


UWEZEKANO wa mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic kurejea kazini Manchester United unazidi kuongezeka kutokana na namna ambavyo mchezaji huyo anazidi kuimarika.

Mshambuliaji huyo alitemwa kwenye kikosi cha Mashetani Wekundu mwishoni mwa msimu wa 2016/2017 baada ya kuumia, lakini kupona kwake kwa kasi kunazidi kuwaduwaza matabibu wa klabu.

Picha zake na video ambazo amekuwa akiposti zikimuonyesha akifanya mazoezi ya aina tofauti yakiwemo ya karate, vinaonyesha ni mtu aliyepona na aliye tayari kurudi uwanjani.

Kuna matumaini makubwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 atarudishwa kikosini Manchester United, lakini mshahara wake utaoungua kutoka Pauni 367,640 alizokuwa anapokea kwa wiki wakati anasaini kutoka Paris Saint-Germain mwaka 2016.

Matarajio ni kurejea ifikapo January na Ibrahimovic mwenye rekodi ya kufunga mabao 17 katika mechi 27 za Ligi Kuu ya England na 28 kwa ujumla, hajasahaulika na hata wakala wake, Mino Raiola ana matumaini hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here