Mwili wa mwalimu huyo wa Ugenya High School ulikutwa katika soko la Sega jana Jumamosi asubuhi na watu waliokuwa wakielekea katika mazishi ya Mkurugenzi wa TEHAMA wa IEBC, Chris Msando, Kijiji cha Lifunga.
Mkuu wa Polisi katika Kaunti ya Siaya, Sarah Duncan amesema uchunguzi unaendelea na upelelezi wa awali unaonyesha kuwa marehemu alibakwa na watu wengi na sehemu zake za siri pamoja na sikio moja kukatwa vibaya.
Familia yake inaeleza kuwa mara ya mwisho alitoka nyumbani siku ya Ijumaa na kwenda kudai malipo yake kwa kazi aliyofanya ya usimamizi wa Uchaguzi Mkuu uliomalizika.
No comments:
Post a Comment