Akiz ungumza baada ya uzinduzi huo, Kaimu M kuu wa mkoa wa Mtwara amba y e ni mkuu wa wilaya ya Mtwara EVODI MMANDA, amewataka wafanyabiashara mkoani humo kuchangamkia fursa za kibiashara huku akitoa msisitizo kwa bidhaa za chakula.
Amesisitiza kuwa vyakula aina ya viazi, nyanya, choroko, mbaazi na bidhaa nyi ngine zote zinapatikana mkoani Mtwara, hivyo wajasiria mali hawana budi kufungasha bidhaa hizo katika ubora unaostaili ili waweze kufanya biashara ya uhakika.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mtwara, Bwana SAIDI SWALLAH amesema kuzinduliwa kwa meli hiyo ni fursa kwa wafanybishara kwani sehemu kubwa ya nchi ya komoro inaagiza chakula kutoka Madagascar ikiwemo nyama ya ng'ombe na mbuzi hivyo ni fursa kwa Tanzania.
Kwa upande wake balozi wa Comoro hapa nchini Dakta AHAMADI FAKHII amesema lengo la Rais wa Comoro na Tanzani ni kuona uchumi wan chi hizo unakuwa kwa kasi, hivyo wafanyabiashara hawana budi kutumia frusa hizo kukuza uchumi wan chi hizo.
No comments:
Post a Comment