Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa, Erasto Philly alisema Mahakama imemtia hatiani mshtakiwa kutokana na ushahidi uliotolewa na shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mwanafunzi.
Hakimu Philly alisema mshtakiwa alitenda makosa hayo Agosti 2017, kwa kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi huyo.
Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Emmanuel John aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kutokana na mshtakiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake ikilinganishwa na wa binti.
No comments:
Post a Comment