Mmoja ajeruhiwa kwenye ajali chamazi - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, September 1

Mmoja ajeruhiwa kwenye ajali chamazi

Na Mustafa Ismail


Shugli za uchukuzi zilisitishwa kwa takriban saa mbili katikaka makutano ya  barabara ya chamazi majimatitu wilaya ya temeke mkoani Dar es salaam baada ya foleni kubwa iliyosabibishwa na ajali iliyohusisha gari aina ya Dcm na kujeruhiwa kwa mtu mmoja.


Ajali hiyoilitokea Maji Matitu Temeke jijini Dar es Salaam leo  asubuhi ambapo daladala hilo pia liliyagonga magari mengine matatu na kuzua kizaazaa katika barabara ya
Mkazi wa eneo hilo Hamisi Juma aliyeshuhudia ajali hiyo amesema ni mungu kasaidia kutokea kwa vifo kwani ajali hiyo ilikuwa ni mbaya sana." Saa 12 na dakika 55 nikiwa nasubiri gari kwenda kazini niliona daladala lililokuwa likitoka Charambe kwenda Chamazi lilikuwa likipita upande ambao si wake likiwa katika mwendo wa kasi na ghafla lililigonga gari dogo namba T 628 DFE ambalo ligeuka na kulala katika mtaro" alisema Juma.

Aidha juma aliongeza kuwa baada ya kuligonga gari hilo liliyaparamia magari mengine madogo mawili yaliyokuwa karibu yake kuku na kuyasukumia kwenye mtaro “Alipogonga tu alishindwa kulidhibiti gari na kuyagonga magari mengine halfu likaangu”
Aliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo dereva wa daladala hilo alikimbia na kulitelekeza gari lake.
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T 628 DFE, T 397 BVB, T 451 CQB na T 458 CAN.
Ajali za mara kwa mara hutokea katika barabara hii ya chamazi huku kidole cha lawama kikielekezwa kwa madereva hususan wa gari za umma almaarufu [daladala] kwa kukiuka alama na sharia za barabarani.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here