ZIDANE HATAKI MBWEMBWE - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, September 14

ZIDANE HATAKI MBWEMBWE

Na Anael James Waziri_Tall


MENEJA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amekataa kukipa nafasi kikosi chake wakati wakijiandaa kutetea taji lao la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kucheza Sporting Lisbon leo usiku.

Ushindi wa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya mahasimu wao wa jiji Atletico Madrid, uliwapa vijana hao wa Santiago Bernabeu taji la 11 la michuano hiyo Mei mwaka huu.

Akihojiwa kama anadhani kikosi chao kinaweza kutetea taji hilo msimu huu, Zidane amesema suala hilo linaweza kuwa gumu kwani kuna timu nyingi zinazoweza kushinda hivyo inabidi wapambane.

Meneja huyo aliendelea kudai kuwa jambo muhimu ni kuhakikisha wanajiimarisha na kushinda kila hatua ili waweze kufikia malengo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here