AZAM KWELI HALI MBAYA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, October 20

AZAM KWELI HALI MBAYA

NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL
Matajiri wa Jiji la Dar es salaam AZAM FC, Timu ambayo ilikuwa tishio kubwa kwa Vigogo wa Soka Nchini Yanga na Simba kwasiku za hivi karibuni na kuleta upinzani mkubwa katika ligi kuu TANZANIA bara, Msimu huu jahazi lao lazidi kutota baada ya Jana kutoka Sare 1-1 na Mtibwa Sugar ukiwa ni mwendelezo wao mbovu wa kutoshinda katika Mechi 6 za VPL, Ligi Kuu Vodacom.

Azam FC, chini ya Kocha toka Spain Zeben Hernandez, sasa wapo kwenye wimbi la Mechi 6 bila ushindi lililoanzia kwa vipigo toka kwa Simba na Ndanda FC, Sare na Ruvu Shooting na kisha kufungwa na Stand United na kufuata Sare na Yanga na hii ya Mtibwa Sugar.
Mechi hii, iliyoanza Jana Saa 1 Usiku huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, ilianza kwa Mtibwa Sugar kufunga Bao Dakika ya Pili tu kupitia Rashid Mandawa na Azam FC kusawazisha katika Dakika ya 11 kupitia Penati ya Himid Mao.
Matokeo hayo yameiweka Mtibwa Sugar Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 16 kwa Mechi 11 wakati Azam FC wapo Nafasi ya 8 wakiwa na Pointi 13 kwa Mechi 10.
Leo VPL itaendelea kwa Mechi 1 ndani ya Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kati ya Vinara Simba na Mbao FC.
MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZA JANA
Jumatano Oktoba 19
Azam FC 1 Mtibwa Sugar 1
Ruvu Shooting 1 Mwadui FC 1
Ndanda FC 1 Mbeya City 1
Tanzania Prisons 2 Stand United 1
Toto Africans 0 Yanga 2
African Lyon 0 Maji Maji FC 2

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here