NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL
Kocha mkuu wa Simba Joseph Omog ameandika rekodi mpya ndani ya klabu
ya Simba msimu huu baada ya kucheza mechi 10 bila kupoteza mchezo wowote.
Msimu wa 2009-2010 Patrick Phiri alioongoza Simba kutwaa taji la ligi kuu Tanzania bara bila kupoteza mechi hata moja.
Abdallah Kibadeni ‘King Kibadeni’ akisaidiana na Jamhuri Kihwelu
‘Julio’ ndiyo makocha wengine walioisaidia Simba kucheza mechi 10 za
mwanzo wa ligi bila kupoteza mchezo katika msimu wa 2013-14.
Katika mechi hizo 10 zilizosimamiwa na Kibadeni pamoja na Julio,
Simba ilifanikiwa kushinda mechi 5 huku mechi 5 nyingine ikitoka sare.
Katika msimu huo, Simba ilipoteza mechi yake kwa mara ya kwanza dhidi ya
Azam FC kwa kipigo cha magoli 2-0 msimu ambao pia Azam walitwaa taji la
gili mwishoni mwa msimu.
Rekodi aliyoweka Omog
Mcameroon huyo amefanikiwa kuiongoza Simba kushinda mechi nane na
kutoka sare mara mbili katika mechi 10 za kwanza tangu kuanzanza kwa
msimu huku Simba ikiwa ni timu pekee ambayo bado haijaonja ladha ya
kipigo hadi sasa. Licha ya kuwa sawa na King Kibadeni kwa kuiongoza
Simba katika mechi 10 bila kupoteza, Omog anabebwa na idadi ya mechi
ambazo Simba imepata ushindi.
Simba ikiwa chini ya Omog imeshinda mechi 8 na kutoka sare katika
mechi mbili wakati wa Kibadeni Simba ilishinda mechi 5 na kutoka sare
katika mechi 5 katika mechi 10 za mwanzoni mwa ligi wakisimama kama
wakufunzi wakuu wa klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi.
Licha ya Simba kuanza vizuri msimu huo, haikufanikiwa kutwaa ubingwa
wa ligi badala yake ikamaliza ligi ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo
huku Azam wakitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza chini ya Omog aliyerithi
mikoba ya Stewart Hall Desemba 2013.
Kwa sasa Simba ipo inaongoza ligi ikiwa chini ya Omog kwa pointi zake
26 baada ya kucheza mechi 10. Omog aliisaidia Azam kutwaa taji la
kwanza katika historia yao msimu wa 2013-14. Je msimu huu ataisaidia
Simba kutwaa taji la kwanza baada ya kupita kavu katika misimu mitano?
Mwishoni mwa msimu wa 2013-14, King Kibadeni na Julio walifutwa kazi
na uongozi wa klabu ya Simba kutokana na klabu hiyo kumaliza katika
nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi na nafasi hiyo kuchukuliwa na
Zdravco Lugarusic.
Licha ya kuwapa ubingwa kwa mara ya kwanza katika historia yao, Azam walimtimua Omog mwaka 2015
baada ya kipigo cha magoli 3-0 ugenini na klabu ya El Merreikh ambacho
kilipelekea Azam kutupwa nje kwenye ligi ya mabingwa Afrika katika hatua
ya awali.
SOURCE:Shafiii
Friday, October 21
Home
Unlabelled
KOCHA SIMBA SC, OMOG KUWEKA REKODI MPYA
KOCHA SIMBA SC, OMOG KUWEKA REKODI MPYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment