CHELSEA YAITOA NISHAI MAN UNITED YA MOURINHO - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, October 23

CHELSEA YAITOA NISHAI MAN UNITED YA MOURINHO

NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL
KLABU YA CHELSEA Leo hii wamefanikiwa kuwafumua mashetani wekundu wa OLD TRAFFORD Manchester United bao  4 kwa 0 Uwanjani Stamford Bridge kwenye Mechi ya  Ligi Kuu England, ambayo ni Mechi ya kwanza kwa Meneja wa Man United Jose Mourinho kurejea Uwanjani hapo tangu afukuzwe Umeneja Chelsea Desemba 2015.

Man United, walishindwa kutumia nafasi walizopata katika lango la Chelsea wakionyesha madoido makubwa katika Mechi yote, walikuwa nyuma 2-0 hadi Mapumziko na Chelsea walipata Bao lao la kwanza sekunde ya 30  tu kupitia kwa mchezaji wao Pedro.
Bao la Pili la Chelsea lilifungwa na Gary Cahill.
Baada ya kurejea kipindi cha Pili, Chelsea walipiga Bao nyingine 2 kwenye Dakika ya 62 kupitia kwa Eden Hazard na 70 goli likifungwa na Ngolo Kante.
Matokeo haya yamewaweka Chelsea Nafasi ya 4 wakati Man United wanabaki Nafasi ya 7.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here