SIMBA HII LAZIMA UTAITAKA TU - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, October 23

SIMBA HII LAZIMA UTAITAKA TU

NA ANAEL JAMES WAZIRI_TAL

Klabu  ya Simba inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara, Leo kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wamefanikiwa kuvunja uteja wao dhidi ya Toto Africans kwa kuicharaza goli 3-0 na kupaa kileleni wakiwa Pointi 8 mbele.

Bao za Simba zilifungwa na Mzamiru, Dakika za 45 na 72 na jingine la Dakika ya 52 la Mavugo.
Hadi sasa Simba ndio wapo kileleni mwa ligi kuu Tanzania Bara sasa wakiwa na Pointi 29 kwa Mechi 11 baada ya kushinda Mechi 9, Sare 2 na Kutofungwa.
Timu ya Pili ni Yanga yenye Pointi 21 kwa Mechi 10 wakifungana na Stand United, waliocheza Mechi 12, lakini wana udhaifu wa Magoli na hivyo kushika Nafasi ya 3.
Mechi ifuatayo ya Simba ni ya Ugenini hapo Oktoba 20 dhidi ya Mwadui FC yenye masikani yake Mkoani SHINYANGA.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here