MIKIKI YA LEO LIGI KUU HISPANIA SOMA HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, October 29

MIKIKI YA LEO LIGI KUU HISPANIA SOMA HAPA

NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL
Weekend ya burudani imewadia tena siku ya leo jumamosi wanaoongoza msimamo wa La Liga Real Madrid wako Ugenini huko Mjini Vitoria, Spain ndani ya Estadio Mendizorroza kucheza na Alaves huku wakiombea Staa wao Cristiano Ronaldo arejee hali ya kutoboa Nyavu kila mara.

Baada ya kusakamwa na Sare 4 mfululizo zilizowapotezea uongozi wao wa La Liga, Real walifyatua Jumla ya Mabao 20 katika Mechi 4 na kurejea kileleni huku pia wakifanya vyema kwenye UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI na Copa del Rey.
Lakini kwenye hizo Bao 20 Ronaldo amefunga 1 tu na sasa ana Bao 4 katika Mechi zake 9 na hayo ni matokeo mabovu mno kwa Supastaa huyo tangu ajiunge na Real Miaka 7 iliyopita.
Lakini Kocha wa Real, Zinedine Zidane, amepooza hali hiyo kwa kusema:“Ningependa yeye afunge Bao 2 au 3 kila Mechi lakini sina wasiwasi najua hali hii itapita tu!”
Zidane anatarajiwa kutumia Kikosi kilekile kilichoifunga Athletic Bilbao Wikiendi iliyopita ambacho kitakuwa na Ronaldo, Bale, Benzema, Marcelo, Mateo Kovacic na Raphael Varane ambao Juzi hawakucheza Mechi ya Copa del Rey waliyoitwanga Cultural Leonesa 7-1.
Alaves wapo Nafasi ya 13 kwenye La Liga baada ya kushinda Mechi 2 kati ya 9 wakiwa La Liga kwa mara ya kwanza Msimu huu baada ya Miaka 10.
Lakini, Alaves, chini ya Kocha aliekuwa Beki wa zamani wa Valencia na Liverpool, Mauricio Pellegrino, Mwezi uliopita waliinyuka Barcelona 2-1 huko Nou Camp na pia kutoka Sare na Atletico Madrid Ugenini huko Vicente Calderon katika Mechi ya kwanza kabisa ya Msimu huu.

Leo Jumamosi Oktoba 29
14:00 Sporting Gijon v Sevilla FC
17:15 Deportivo Alaves v Real Madrid CF
19:30 Atletico de Madrid v Malaga CF
21:45 FC Barcelona v Granada CF

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here