wananchi wanakiu ya maendele:Magufuli - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, November 2

wananchi wanakiu ya maendele:Magufuli

Na Mustafa Ismail
Kenya 
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema viongozi wa Afrika Mashariki wameamua kufanya kazi ya kuharakisha maendeleo na kuinua maisha ya wananchi.


rais kenyata wa kenya na Magufuli wa tanzania wakizinduz barabara mcepuko ya  southern bypass jijini Nairobi
Amesema hiyo ndiyo ndiyo maana wamedhamiria kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara zinazounganisha nchi wanachama na kujenga vituo vya pamoja vya utoaji wa huduma za mpakani.
Wananchi wanahitaji maendeleo na haya ndio maendeleo, barabara hii itasaidia kuinua uchumi na itasaidia masuala ya kijamii" amesema Rais Magufuli, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya Tanzania.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa barabara ya mchepuko ya Southern By-pass jijini Nairobi, Rais Magufuli alisema barabara hiyo sio tu itawasaidia wananchi wa Kenya bali pia itawasaidia wananchi wa Afrika Mashariki wanaotumia barabara zinazopitia Nairobi.
Barabara hiyo ya urefu wa kilomita 29 imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Nairobi.

Ujenzi wa barabara hiyo umegharimu dola 187 milioni za Kimarekani ambazo, sehemu yake ilitolewa kama mkopo na Serikali ya China kupitia benki yake ya Exim.

Rais Magufuli, ambaye anamaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Kenya leo, alizindua barabara hiyo akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais Kenyatta amesema Kenya itaongeza juhudi katika utekelezaji mradi wa ujenzi wa barabara zinazounganisha Kenya na Tanzania zikiwemo barabara ya Malindi kupitia Saadani hadi Bagamoyo nchini Tanzania na barabara ya Voi - Taveta- Horiri-Arusha.

Kabla ya kuzindua barabara hiyo Rais Magufuli alitembelea kiwanda kidogo cha kusindika maziwa cha Eldoville eneo la Karen, Nairobi.
Kiwanda hicho kinamilikiwa na familia ya mkulima Bw James Karuga. ambayo ilianzisha kiwanda cha kusindika maziwa mwaka 1985 kwa uzalishaji wa chini ya lita 1,000 kwa siku.

Kwa sasa kiwanda hicho kimefikia uzalishaji wa lita 5,000 kwa siku na familia hiyo inatarajia kuongeza uzalishaji hadi lita 70,000 katika mwaka mmoja ujao.

ziara ya rais wa Tanzania nchini kenya inalengwa kuwa na mafanikio makubwa na kufungukwa kwa soko zaidi la biashara na kuzidisha uhusiano mwema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here