MOURINHO:KUMUUZA ROONEY MSAHAU - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, October 23

MOURINHO:KUMUUZA ROONEY MSAHAU

NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL
Licha ya kupoteza mchezo dhidi ya Chelsea,Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameapa kamwe hatamuuza nahodha wa  timu yake Wayne Rooney.

Hivi sasa Rooney amekuwa hana namba ya kudumu ndani ya Kikosi cha Man United na katika Mechi 3 zilizopita za EPL, Ligi Kuu England, ameingizwa kutokea Benchi.
Lakini Mourinho anaamini hadhi ya Rooney kama mmoja wa Wachezaji Bora katika Historia ya Man United, baada kuichezea Mechi zaidi ya 500 na kukaribia Mabao 250 ambayo yatakuwa ni Rekodi, itakuwa ni uamuzi wake mwenyewe Rooney kuendelea kuichezea Klabu hiyo au la.
Mourinho ameeleza: "Sitafanya uamuzi huo. Mchezaji wa hadhi hiyo, Mchezaji wa Historia kubwa kwa Klabu, haitafika wakati ambapo Klabu au Meneja kuamua kwa niaba yake!"
Alifafanua: "Nilimweka benchi Mechi 3 mfululizo. Ni ngumu kwake, ngumu kwangu, ni ukatili lakini ni maslahi ya Timu. Kumweka benchi Lejendari ni ngumu!"
Mourinho amesema yeye anadhani matatizo ya Rooney ya hivi sasa yameanza kutokana na kumbadili mno pozisheni za kucheza katika Misimu ya hivi karibuni na yeye anaamini nafasi bora kwa Rooney ni kucheza Fowadi mbele kabisa.
Klabuni Man United na Timu ya Taifa ya England, mara nyingi Rooney amekuwa akitumiwa kama Kiungo na Mourinho ameeleza: "Hilo limeleta kutojiamini kuhusu wapi ndio anafaa na nini hatima yake ya baadae. Anakuwa hatulii kimawazo. Mara Namba 6 kwenda 9 au 9 kuwekwa 10 au 9 kurudishwa 6. Kwangu mimi yeye ni Mchezaji wa Kushambulia. Yeye ni 9 au 10!"
Pia Mourinho alikataa kuunga mkono msimamo kuwa Rooney amekwisha na kudai atarejea kwenye hali yake ya kawaida kwa Klabu yake na England.
Amesema: “Nadhani anaandamwa kwa mafanikio yake. Alipata mafanikio makubwa sana katika Maisha yake ya Soka. Aliinua matarajio ya Watu kwa kiwango kikubwa mno kiasi ambacho Watu sasa wanadai awe hivyo hivyo kila Mechi, kila Wiki, kila Mwezi, kila Msimu kwa kiwango hicho hicho cha juu kabisa. Kwangu mimi hilo ndio tatizo!”.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here