AHADI ZA TRUMPLE NDANI YA SIKU 100 - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, November 9

AHADI ZA TRUMPLE NDANI YA SIKU 100

NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL

Katika historia ya Marekani hakujawahi kutokea Raisi wa aina ya Donald Trumple mwenye jina kubwa katika ufanya biashara na ujasiliamali kwa ujumla.
Rais Mpya wa Marekani Donald Trumple

Matamshi yake yenye utata na msimamo mkali kuhusu uhamiaji, vilileta msukosuko ndani ya chama chake na mgawanyiko nchini.

Lakini ahadi yake ya "kuiweka mbele nchi "iliwavutia mamilioni ya waamerika ambao wanahisi kuhujumiwa na mfumo wa sasa.


 Kwa hivyo ni kipi tunatarajia kutoka kwa bwana Trump?

Baadhi ya ahadi zake ndani ya siku 100 za kwanza zilitolewa wakati wa hotuba yake mwezi uliopita mjini Gettysburg jimbo la Pennsylvania.

Ameapa kujenga ukuta kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico, mradi ambao utagharamiwa na Mexico.

Ahadi nyingine ambayo licha ya kutokuwepo kwenye hotuba ya Gettysburg ni kusaini upya mikataba ya biashara kati Marekani,Canada na Mexico.

Anasema kuwa mikataba hii inachangia katika kuwapokonya raia ajira zao.

Trump pia ameahidi kuboresha uhusiano na Raias wa Urusi Vladimir Putin, ambaye amemsifu na kumtaja kuwa kiongozi aliye imara.

Aidha ameapa kuondoa Marekani kutoka kwa mkataba kuhusu mpango wa nuklia wa Iran.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here