BAADA YA UEFA CHAMPIONS LEGUE LEO MAN UNITED NA TIMU YA SAMMATA DIMBANI,ANGALIA NA RATIBA YA EUROPA CHAMPIONS LEGUE - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, November 24

BAADA YA UEFA CHAMPIONS LEGUE LEO MAN UNITED NA TIMU YA SAMMATA DIMBANI,ANGALIA NA RATIBA YA EUROPA CHAMPIONS LEGUE

Na Anael James 
MANCHESTER UNITED Leo wanatinga Uwanjani kwao Old Trafford kucheza Mechi yao ya 5 ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI wakisaka ushindi ili kujiweka hai kwenye 2 Bora ambazo zitaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 32.

Image result for man united vs feyenoord

Hii ni moja ya Mechi zote za 5 za Makundi zinazochezwa Leo na baada ya hii kila Timu itabakiza Mechi 1 tu itakayochezwa Desemba 8.
Kwenye Kundi A, Man United wapo Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Fenerbahce wenye Pointi 7 kama vile Feyenoord.
Man United, ambao wameshinda Mechi zao zote 2 za Kundi A walizocheza Old Trafford na Fenerbahçe na Zorya Luhansk, Leo wanacheza na Feyenoord ambayo, bila kutegemewa, iliifunga Man United 1-0 huko Rotterdam Mwezi Septemba kwenye Mechi ambayo Man United na walistahili kushinda.

Image result for man united vs feyenoord

Meneja wa Feyenoord, Giovanni van Bronckhorst, Mchezaji wa zamani wa Arsenal, anaihofia Man United akitegemea kusulubiwa na hata fomu ya Timu yake sio nzuri kama mwanzoni mwa Msimu waliposhinda Mechi zao 11 za kwanza kati ya 12, moja ikiwa dhidi ya Man United.
Lakini hivi karibuni wameshinda Mechi 1 tu kati ya 5 ingawa Wikiendi iliyopita waliipiga 3-0 PEC Zwolle kwenye Ligi ya kwao Holland.
Wakati Feyenoord itawakosa Terence Kongolo na Eric Botteghin kutokana na Majeruhi na kufungiwa, Man United Majeruhi wao ni Eric Bailly na Chris Smalling wakati ipo hatihati kwa Marouane Fellaini kucheza kutokana na Musuli za Mguu kumsumbua.
Meneja wa Man United, Jose Mourinho, anatarajiwa kubadili Kikosi toka kile kilichotoka 1-1 na Arsenal na mmoja wa Wachezaji ambao watacheza hii Leo ni Henrikh Mkhitaryan ambae amekuwa hachezeshwi na pia Zlatan Ibrahimovic alieikosa Mechi na Arsenal kwa kuwa Kifungoni.
VIKOSI:
Man United: De Gea – Valencia, Jones, Bailey, Rojo – Pogba, Herera – Mata, Rooney, Mkhitaryan – Ibrahimovic
Feyenoord: Jones – Van der Heijden, Nelom, Botteghin, Karsdorp – El Ahmadi, Kujit, Vilhena – Elia, Jorgensen, Toornstra
REFA: Manuel Gräfe (Germany)

RATIBA YA GAME NYINGINE
KUNDI A
19;00 Fenerbahçe v Zorya Luhansk         
23;05 Manchester United v Feyenoord              
KUNDI B
19;00 FC Astana v Apoel Nicosia  
23;05 Olympiakos v BSC Young Boys                
KUNDI C
1900 FK Qabala v RSC Anderlecht          
2305 Saint-Étienne v Mainz 05              
KUNDI D
1900 Zenit St Petersburg v Maccabi Tel-Aviv              
2305 Dundalk v AZ Alkmaar        
KUNDI E
23;05 Austria Vienna v Astra Giurgiu                
23;05 Roma v Viktoria Plzen                  
KUNDI F
23;05 Athletic Bilbao v Sassuolo             
23;05 KRC Genk v Rapid Vienna             
KUNDI G
21;00 Ajax v Panathinaikos          
21;00 Celta Vigo v Standard Liege          
KUNDI H
21;00 KAA Gent v Sporting Braga           
21;00 Shaktar Donetsk v Konyaspor                 
KUNDI I
21;00 FC Schalke 04 v Nice          
21;00 FK Krasnodar v FC Red Bull Salzburg                 
KUNDI J
21;00 Fiorentina v PAOK Salonika           
21;00 Slovan Liberec v FK Qarabag                  
KUNDI K
21;00 Hapoel Be'er Sheva v Inter Milan            
21;00 Sparta Prague v Southampton                
KUNDI L
21;00 FC Zürich v Villarreal
21;00 Steaua Bucharest v Osmanlispor        

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here