chapisho la kumfananisha mke wa obama na sokwe lazua hisia kali - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, November 15

chapisho la kumfananisha mke wa obama na sokwe lazua hisia kali

Na Mustafa Ismail
Chapisho la kibaguzi kuhusu mke wa rais wa Marekani Michelle Obama limezua utata unaomuhusu meya wa jimbo la Virginia.
Pamela Ramsey Taylor ,ambaye anaendesha shirika moja la kihisani katika kaunti ya Clay, alimfananisha Michelle Obama na 'sokwe' .
 'Itakuwa vyema kuwa na mtu anayefuata mitindo,mrembo na mke wa kwanza mwenye heshima.Nimechoka kuona sokwe lililovaa viatu'',alisema.
Meya mwengine kutoka eneo hilo Beverly Whaling alijibu kwa kusema ''umeifanya siku yangu nzuri''.
Bi Beverly Whaling ni meya wa mji wa Clay ambao una idadi ya takriban watu 491.Mji huo hauna wakaazi wa Marekani wenye asili ya Kiafrika,kulingana na idadi ya watu iliotolewa 2010.
chapisho la facebook lililomfananisha bi michael obama na sokwe
Katika kaunti ya Clay zaidi ya asilimia 98 ya wakaazi 9,000 ni watu weupe.
Licha ya idadi hiyo ndogo katika jimbo hilo ,chapisho hilo la facebook lilisambaa nchini Marekani na katika vyombo vya habari vya kimataifa huku ombi la kuwataka wanawake wote wawili kufutwa kazi likikusanya saini 85,000.

Gazeti la The Washington post na lile la New York Daily yaliripoti kwamba bi Taylor aliondolewa katika wadhfa wake siku ya Jumatatu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here