KOCHA WA TIMU YA TAIFA BRAZIL ATOA NENO KUELEKEA KOMBE LA DUNIA NCHINI URUSI - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, November 29

KOCHA WA TIMU YA TAIFA BRAZIL ATOA NENO KUELEKEA KOMBE LA DUNIA NCHINI URUSI

                              Image result for TITE

KOCHA wa Brazil Tite amesema Kikosi chake kinakaribia kuwa na hakika na kufuzu kwa safari ya kwenda Russia kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018.
 
Tangu atwae wadhifa kutoka kwa Dunga Mwezi Juni, Tite aliitoa Brazil kutoka Nafasi ya 6 ya Kundi la Nchi 10 za Kanda ya Marekani ya Kusini kwa kushinda Mechi zao zote 6 wakifunga Bao 17 na kufungwa 1 tu na kukamata Nafasi ya Kwanza ya Kundi hilo wakiwa na Pointi 27 kwa Mechi 12.
Nchi 4 za juu za Kundi hilo lenye Nchi 10 zitafuzu moja kwa moja kwenda Russia na ya 5 kutinga Mechi ya Mchujo ili kusaka nafasi ya kufuzu.
Akiongea hapo Jana kwenye Mahojiano maalum,  Tite alisema ameshangazwa na Timu kubadilika kutoka lile janga la kubandikwa 7-1 kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Dunia na Germany kwenye Mechi iliyochezwa Nchini kwao Mwaka 2014.
Tite amesema: "Tunajenga msukumo mpya kwa Timu ya Taifa. Tunaijenga Timu ili tufuzu kwa kucheza Soka safi lenye tija."
Mwezi Machi Brazil wataenda Ugenini kucheza na Uruguay na ushindi huko utawaweka karibu ya kufuzu na kudumisha ile rekodi yao ya kuwa Nchi pekee Duniani iliyocheza kila Fainali ya Kombe la Dunia.
Kabla ya Tite kutua Brazil, Timu hiyo maarufu kwa wenyewe kama Selecao, ililaumiwa sana kwa kumtegemea mno Neymar lakini sasa mbali ya Fowadi huyo wa Barcelona wapo Vijana wengine wanaoibeba vizuri mno wakiwamo Philippe Coutinho na Gabriel Jesus.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here