LADY JAY DEE KIFUNGONI - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, November 2

LADY JAY DEE KIFUNGONI

NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL

Mwanamuziki nyota wa kike nchini Tanzania Judith Wambura maarufu Lady Jay Dee amefikishwa katika mahakama ya kinondoni jijini Dar es salaam kutokana na tuhuma nzito zinazomkabili kwa kosa la kutoa maneno yasiyokuwa na maadili (machafu) dhidi ya Ruge Mtahaba na Joseph Kusaga.



Mahakama hiyo ya wilaya ya Kinondoni imemtaka msanii huyo mwanadada Jay Dee aombe radhi kupitia kwenye vyombo vya habari vyenye wigo mpana hapa nchini Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania.

Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashtakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga kwa kuuchafua uongozi wa kampuni hiyo na viongozi wake kupitia mitandao ya kijamii katika malumbano makali kati ya pande hizo mbili.

Mnamo mwezi Mei 2013, Kituo cha habari "Clouds Media Group na Ruge walimburuza Jay Dee mahakamani kwa kile walichodai kwamba alikuwa akiwatukana kwenye mitandao ya kijamii".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here