MPYAAA:MASHABIKI WA MANCHESTER WATAKA FA IMUADHIBU REFA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, November 2

MPYAAA:MASHABIKI WA MANCHESTER WATAKA FA IMUADHIBU REFA

NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL


MARA baada ya FA, Chama cha Soka England, kuamua kumfungulia Mashitaka Meneja wa Manchester United Jose Mourinho baada ya Refa Mark Clattenburg kumtoa Uwanjani Jumamosi iliyopita wakati Timu yake ikitoka 0-0 na Burnley, Mashabiki wa Klabu hiyo wamekuja juu.


Image result for mourinho


Mashabiki hao wanataka Refa huyo nae achukuliwe hatua kwa makosa yake na historia yake mbovu.
Hii si mara ya kwanza kwa Clattenburg kukwaruzana na Man United kwani Miaka 9 iliyopita Sir Alex Ferguson alimvaa na kumbatukia wakati wa Haftaimu huko Reebok Stadium walipocheza na Bolton Wanderers.


Ferguson alichukizwa na Refa huyo kwa kutomchukulia hatua yeyore Kevin Davies aliekuwa akimwandama Patrice Evra kwa rafu za makusudi.


Clattenburg hakumpa Kadi yeyote Davies na badala yake kumtimua Ferguson kutoka Benchi na kulazimika kukaa Jukwaa la Watazamaji kwa Kipindi cha Pili chote.


Baada ya Mechi hiyo Ferguson alieleza: "Nilimwambia Refa nini ninachofikiri. Marefa wengine hawapendi hilo. Hawapendi ukweli. Lakini nilinwambia alikuwa mbovu Kipindi cha Kwanza!"


Hali kama hiyo sasa inemkuta Mourinho ambae alichukizwa na Refa huyo kuinyima Man United Penati ya wazi na sasa anakabiliwa na Kesi ambayo Adhabu yake inaweza kuwa Onyo, Faini, Kufungiwa kukaa Benchi au kupigwa marufuku kukanyaga Uwanjani.


Upo wakati Refa Clattenburg alipokumbana na hasira za Mashabiki wa Man United ambao baada tu Refa huyo kuwatoa nje kwa Kadi Nyekundu Wachezaji Wawili wa Man United wakati wanaifunga Chelsea huko Stamford Bridge, waliinua Bango kubwa la kebehi liloandikwa: "CLATTENBURG REFA, KIONGOZI, LEJENDARI'.


Katika Miaka Mitano iliyopita, Clattenburg ameshawapa Kadi Nyekundu lundo la Wachezaji wa Man United ambao ni Jonny Evans, Nemanja Vidic, Tyler Blackett, Luke Shaw na Chris Smalling.


Mwezi Septemba, Mourinho alimlaumu Clattenburg kwa kushindwa kumpa Kadi Nyekundu Kipa wa Man City Claudio Bravo kwa kumwangusha Wayne Rooney kosa ambalo pia lilistahili Penati ambayo haikutolewa.


Refa Clattenburg aliwahi kukaa Minne na Nusu bila kuchezesha Mechi ya Everton baada ya 'kuiminya' kwenye Dabi ya Merseyside walipocheza na Liverpool Mwaka 2007 na Everton kulalamika mno juu yake.


Nae Refa wa zamani wa Ligi Kuu England, Graham Poll, amemponda mno Clattenburg kwa uchezeshaji wake wa Mechi hiyo na Burnley iliyomtia matatani Mourinho.
Poll amebainisha kuwa Man United walistahili Penati baada ya Matteo Darmian kuangushwa ndani ya Boksi na Jon Flanagan.


Pia Refa huyo wa zamani alitoboa kuwa Clattenburg alikosea kumpa Kadi ya Njano ya Pili Ander Herrera na hivyo kumtoa kwa Kadi Nyekundu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here