MPYAAA :KIKOSI CHA ENGLAND KINACHOIVAA SCOTLAND - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, November 7

MPYAAA :KIKOSI CHA ENGLAND KINACHOIVAA SCOTLAND

NA ANAEL NJAMES WAZIRI_TALL

Meneja  BOSI wa England, Gareth Southgate, ametangaza Kikosi cha Wachezaji 25 cha kuivaa Scotland Ijumaa Uwanjani Wembley kwenye Mechi ya Kundi F la Nchi za Ulaya zinazowania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

 
England pia itaivaa Spain Jumanne Novemba 15 kwenye Mechi ya Kirafiki.
Miongoni mwa hao 25 ni Jack Wilshere na Harry Kane ambao wamerejeshwa tena Kikosini.
Wilshere, Kiungo wa Miaka 24 wa Arsenal, aliachwa Mechi 2 zilizopita lakini tangu aende kwa Mkopo huko Bournemouth fomu yake imepanda.
 
Nae Straika wa Tottenham Harry Kane ambae alizikosa Mechi 2 za England baada kuumia Enka yupo tena kundini baada kupona.
Wawili wa Manchester United, Chris Smalling na Luke Shaw, hawamo Kikosini kutokana na kuumia.

KOMBE LA DUNIA 2018
Mchujo Nchi za Ulaya
KUNDI F
Baada Mechi 3, Msimamo:
-England Pointi 7
-Lithuania 5
-Slovenia 5
-Scotland 4
-Slovakia 3
-Malta 0

Pia Kiungo wa Spurs Dele Alli hayumo baada kuumia Goti mazoezini kabla ya Mechi ya Jana ambayo Tottenham ilitoka 1-1 na Arsenal.
 
Nae Beki wa Burnley,  Michael Keane, ambae alianzia Soka lake huko Man United, amebaki Kikosini kufuatia kuitwa kwa mara ya kwanza Mwezi uliopita kuziba pengo la Majeruhi.
 
Pia, baada kupona maumivu yao, Nathaniel Clyne, Adam Lallana na Raheem Sterling wamo Kikosini.
England - Kikosi kamili cha Wachezaji 25: Forster (Southampton), Hart (Torino), Heaton (Burnley); Bertrand (Southampton), Cahill (Chelsea), Clyne (Liverpool), Jagielka (Everton), Keane (Burnley), Rose (Tottenham), Stones (Man City), Walker (Tottenham); Dier (Tottenham), Drinkwater (Leicester), Henderson (Liverpool), Wilshere (Bournemouth), Lallana (Liverpool), Lingard (Man Utd), Rooney (Man Utd), Sterling (Man City), Townsend (Crystal Palace); Walcott (Arsenal), Kane (Tottenham), Rashford (Man Utd), Sturridge (Liverpool), Vardy (Leicester).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here