Rais Magufuli: Niwashukuru sana kwa michango yenu
mikubwa katika maeneo yenu ya kazi.
Swali(Tido Mhando): Ulichukua muda kuunda baraza la
mawaziri, Je Katika tathmini hiyo wanafanya kazi kulingana na ulichotegemea
wakifanye
Jibu(Magufuli): Serikali niliyounda imenisaidia sana
na wanafanya kazi zao vizuri, niliona niwe na baraza la watu wachache katika
kuwatumikia wananchi, changamoto zipo lakini nina imani kubwa.
Swali(Lulu Sanga TV 1): Kuna changamoto kubwa sana ya
dawa, watoto wengi wanakufa kutokana na kukosa dawa, unaoneje ukibana matumizi
kupata dawa ukazigawa hospitali kubwa au kampeni kama ile ya madawati.
Jibu(Rais Magufuli): Katika bajeti yetu tumetenga
bilioni 1.99 na tumeongeza bajeti ya kununulia madawa karibu mara kumi.
Tumebadilisha utaratibu badala ya kununua kutoka kwa suppliers sasa tunanunua
moja kwa moja kutoka viwandani pia kuna nchi zinataka kuwekeza kujenga viwanda
vya kutengeneza madawa hapahapa.
Swali kuhusu kukandamiza demokrasia:
Jibu: Katika kazi yoyote Sijakandamiza demokrasia
ndio maana unaona bunge linaendelea na chaguzi zinaendelea hata hapa wamechagua
UKAWA, demokrasia ina mipaka yake, baada ya uchaguzi lazima watu waendelee na
production
Swali(Tido)-Nyongeza: Kuna watu wanasema unataka
kuelekea kwenye udikteta
JIBU: Tafsiri kila mmoja ana yake na kila mmoja ana
uhuru wa kufukiria anavyofikiria hata wewe Tido ulihama BBC, TBC na sasa uko
Azam, mwingine anaweza kufikiri uko ulikokuwa kulikuwa na udikteta wa aina
fulani.
Swali(Rioba): Unasisitiza uchumi wa viwanda, Tanzania
imeshawahi kuwa na viwanda vikafa, kuna watu wanaona hili swala waachiwe watu binafsi,
wewe unaoneje?
Jibu: Ilani inasema tunataka kujenga nchi ya viwanda,
huwezi kutegemea serikali katika kujenga viwanda ndio maana nikasema kuna
makampuni kutoka Kenya na sio makampuni ya watu binafsi.
Swali(Mtanzania): Serikali imeweka mkazo kwenye
kupambana na majangili lakini tishio ni kubwa,
Jibu(Rais Magufuli): Umezungumza ukweli na ni changamoto ila
pia ina historia yake, sheria ya mifugo ya mwaka 59 ila tumejipanga kuhakikisha
haya masuala yasije yakawa parmanent na tumeibadilisha wizara ya maliasili na
nimeteua majenerali kuongoza wizara nadhani umeshajua tunataka kufanya nini.
Hatuna viwanda vya nyama nchi hii ndio maana mifugo haina pakwenda.
Swali(Magazeti ya serikali): Ni nini mkakati wa
kuwafanya watanzania kuona fursa katika sekta nyingine
Jibu(Rais Magufuli): Sisi kama serikali ni
kuwaelimisha waweze kutumia fursa zilizopo katika nchi nyingine, mfano sisi
tunasifika kwenye Kiswahili, kila mmoja ajipange badala ya kusubiri serikali.
Fursa zipo ikiwemo EAC na SADC ambako Tanzania ni mwanachama. Ni wajibu sisi wa
watanzania kuchangamkia fursa.
Swali(Tido Mhando): Ulitilia mkazo Rushwa na ufisadi,
mwaka mmoja sasa unasemaje?
Jibu(Rais Magufuli): Matunda yameanza kuonekana,
nidhamu kazini imeanza kuonekana, tumepitisha sheria ya mafisadi na kesi ya
kwanza imeanza kusikilizwa jana. Rushwa na swala mtambuka na haliwezi
kushughulikiwa na Rais peke yake. Nitoe wito kwa watanzania wote tukatae
Rushwa, ni kansa ya maendeleo.
Swali(Rioba): Kuna maswala umeyasimamia kwa ujasiri
ikiwemo ujangili na dawa za kulevya, nini kinakuumiza kichwa
Jibu(Rais Magufuli): Yanayoniumizwa kichwa ni mengi
pamoja na swali lako, yale niyoahidi katika miaka mitano bado sijayamaliza na
hayawezi kumalizika ndani ya mwaka mmoja. Kwenda mbele unahitaji support ya
watu wengi. Mwenyezi Mungu pamoja na support ya watanzania.
Swali(Tuma-Radio Tumaini): Hongera sana, Kura yangu
ilifanya kazi, Walemavu wa chini hali bado ni mbaya, tunazo sheria nyingi
tunaishukuru serikali. Mazingira yetu(walemavu) bado ni magumu, tunaomba watu
wa chini watu iwaangalie.
Jibu(Rais Magufuli): Nimelipokea ombi lako na
tutaendelea kulishughulikia na serikali inajali sana walemavu kwani hata sisi
ni walemavu wa kesho, nimeunda wizara maalum ya walemuavu, nimewateua walemavu
katika baraza langu ikiwemo Dr Possy, Amon Mpanju.
Swali(Bakari Machumu Mwananchi): Viwanda na utajiri
wa madini, umeelezea umuhimu wa PPP, kuna wafanyabiashara wanahisi wanatengwa,
upande wa madini, tunaunganisha vipi
Jibu(Rais Magufuli): Wafanyabiashara hawajatengwa na
tunawahitaji sana, na mimi nawapenda kweli wafanyabiashara lakini nataka
wanaolipa kodi. Mfanyabiashara ambae hajalipa kodi anawaumiza ambao wamelipa
kodi, ukishakua na wafabiashara wa aina mbili unawaumiza wanaolipa. Palikuwa na
mamabo ya hovyo, sitaki kwenda kwenye detail sana maana mambo mengine yapo
mahakamani, wafabiashara matapeli siwapendi.
Jibu(Rais Magufuli): Kuhusu madini, ni kweli nchi hii
ina madini mengi sana, madini yanatakiwa kunufaisha nchi hii, siku moja
yatakwisha, nina uhakika sasa mambo yataanza kwenda vizuri baada ya kusaini
regulations. Sisi tuna mafuta pia, tutaunganisha bomba la hoima kwenda Tanga,
Tanzanite inapatikana Tanzania tu lakini nchi iliyoongoza kuuza ni India
ikifuatiwa na Kenya.
Sasa hivi umeanzishwa mnada hapa. Watu wanasafirisha
makontena kwenda nje kusafishwa na sisi wenyewe tunayasindikiza. Kwa nini
tusitengeneze hapa, haya ndio ndio najaribu kuyazungumza ili nchi yetu
isiendelee kuibiwa, kwenini kila sehemu kwenye madini kuna kiwanja cha ndege,
hili sio suala la Rais pekee ili pesa zinazopatikana ziwanufaishe watanzania
wote. Unachosema ni sawa na kinachotakiwa sasa kusonga mbele.
Swali(Joseph Kulambwa): Tanzania ya viwanda, serikali
imejipangaje kutrain mafundi mchundo kuliko wasimamizi wa viawanda
Jibu(Rais Magufuli): Vyuo vya kati tulivibadilisha
kuwa vyuo vikuu, ilikua bad direction ndio maana sasa tunajenga vyuo vya VETA
ikiwezekata kila mkoa. Hata chuo cha usafirishaji kimekua chuo kikuu na
inawezakana kwa sababu kulikua na mikopo ambayo hairudishwi ndio maana sasa
kuna deni la trilioni 3.5.
Swali: Wafanyakazi hewa wameondolewa lakini bado mishahara
inayolipwa ni mikubwa?
Jibu(Rais Magufuli): Siku za nyuma kuna madai mengi
ambayo yamepelekea serikali kulipa kiasi cha bilion 22.6 na bado kuna madai
39,000 yenye thamani ya sh bilioni 23
Suala la OC bado halitakuwepo kwani mambo yanaenda vizuri.
Aidha serikali itaendele kulipa madeni ya walimu na
wakandarasi wanaodai.
Swali(Angalieni Mpendu): Suala la utamaduni na
maadili, umeliwekaji katika utawala wako?
Jibu(Rais Magufuli): Jukumu la ku-maintain utamaduni
wetu ni la kila mtanzania, kuna wizara inayoshughulika suala hili. Kila
mtanzania ana wajibu wa kutunza utamaduni wetu.
Vyombo vya habari vitoe ushrikiano kwa kuhakikisha utamaduni
wetu unakuwa mzuri.
Swali(Bukuku): Serikali ya china na Tanzania ni
Marafiki, Unaonaje kama ungefanya mazungumzo ma Wachina kukawa na ushirikiano
katika mafunzo na mashine ndogondogo?
Jibu(Rais Magufuli): Nimeshazungumza nao, wachina
wamekubali na wanataka kuchukua eneo la Bagamoyo wajenge viwanda 1000. Pia
tumezungumza na serikali ya India katika suala kama hilo hilo. Tumezungumza na
serikali ya Morocco na kutakuwa na ndege ya moja kwa moja kutoka Kasablanca
hadi JNIA.
Tumeweka fedha katika benki ya TIB kwa ajili ya kukopesha
wajasiriamali. Tatizo ni kwamba watu wanakopa lakini hawarudishi ikiwemo
wanasiasa. Tatizo la waandishi wa habari hawaaniki watu hawa.
Swali(Tido Muhando): Mchakato wa katiba Mpya umefikia
wapi?
Jibu(Rais Magufuli): Katika kampeni yangu hakuna
sehemu ambayo nimezungumzia suala la Katiba Mpya, hata hivyo suala la katiba
mpya limefika mahali pazuri lakini niacheni kwanza ninyooshe nchi.
Swali(Edoni Mwanika): Kwa nini miswada ya habari
inakuwa haipewi muda wa kutosha kujadiliwa na huletwa kidharura tu?
Jibu(Rais Magufuli): Sheria yeyote ina misingi yake,
mchakato wa sheria hizi umeanza toka mwaka 2010 hadi mwaka huu, hakuna muda
sahihi ungetosha kujiandaa.
Hata hivyo hili ni suala ambalo lipo ndani ya maamuzi ya
bunge hivyo siwezi kuingilia,
Punde musuada huu utakaponifikia nitaisaini na kama ni
marekebisho yatafuata.
Swali(Frank): Umeokoa kiasi gani kwa kutosafiri nje?
umechukua hatua gani kuhakikisha ukanda wa Afrika mashariki unakuwa salama?
Suala la diaspora kutoweza kuwa tena raia wa Tanzania unalizungumziaje?
Jibu(Rais Magufuli): Fedha tulizookoa ni mabilioni,
hata hivyo siyo kwamba hatusafiri kabisa ila tunahakikisha kunakuwa na
uwakilishi ambao unapunguza gharama.
Tumekuwa tunashughulikia migogoro inayoendelea, DRC
nimemtuma mwenyekiti wa mawaziri kwenda ili kutafuta suluhu. Suala la migogoro
linadiliwa mezani, Burundi tumemteua Mh Mkapa na anasuluhisha na mambo yanaenda
vizuri.
Kuhusu diaspora lipo kisheria zaidi.
Swali(Sanga): Una maoni gani katika ishu ya Zanzibar
na Utawala bora?
Jibu(Rais Magufuli): Hali ya Zanzibar ni nzuri,
wamefanya uchaguzi wao vizuri na Dr Shein anafanya vizuri na mambo yanaenda
vizuri
Swali(Manyere): Upi ni msimamo wetu kuhusu Morocco;
Je Ikulu haiwezi kuandaa tuzo kwa waandishi wanaondika mambo mazuri kuhusu
nchi?
Jibu(Rais Magufuli): Tanzania ni nchi isiyofungamana
na upande wowote na hivyo tuna uhuru wa kushirikiana na nchi yeyote.
Hata hivyo Moroco tunashirikiana nao katika kukuza biashara
Vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri kwelikweli,
Nashirikiana na kila mtu hata Masoud anavyonichora kichwa
kimevimba hapa, nashirikiana naye.
Swali(Pasco Mayala): Ulitumia mamlaka gani kuamuru
bunge na mahakama kufanya unayoyataka? ulitumia mamlaka gani kuzuia mikuatana
ya kisiasa?
Jibu(Rais Magufuli): Serikali ndiyo inahusika na
kugawa fedha zote kupitia bajeti, fedha zikitumika vibaya anayehusika ni
serikali.
Swali: Unalizungumziaje suala la ajira? Umekuta mambo
yapoje ikulu? Na ulikuwa unatazamia nini
Jibu(Rais Magufuli): Ajira zilikuwa hazijazuiliwa,
serikali imetoa ajira za madaktari na manesi wa hospitali ya Rweganzira.
Zuio la ajira lilikuwa la muda tuu. Mpaka sasa kuna benki
iliyorudisha fedha za wafanyakazi hewa kiasi cha shilingi bilioni 6.7.
Serikali inaajiri kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha suala
la wafanyakazi hewa
Serikali imeajiri zaidi za watumishi 5000 kwenye vyombo
mbalimbali.
Serikali inaendelea kuboresha maslahi ya wakulima kwa mfano
wa korosho; Kilo ya korosho imeongezeka bei kutoka shilingi 600 hadi sh 4000.
No comments:
Post a Comment