NDEGE ILIYOBEBA WACHEZAJI WA BRAZILI YAPATA AJALI NCHINI COLOMBIA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, November 29

NDEGE ILIYOBEBA WACHEZAJI WA BRAZILI YAPATA AJALI NCHINI COLOMBIA



                     Mabaki ya ndege
Ndege iliyobeba watu 81, wakiwemo wachezaji wa klabu moja ya soka ya Brazil, imeanguka eneo la Medellin nchini Colombia.

Maafisa wanasema watu sita wamenusurika.
Ndege hiyo inadaiwa kupata hitilafu za mfumo wake wa umeme.

 Ndege hiyo ilianguka eneo lenye milima mingi ikielekea Medellin
Ndege iliyobeba watu 81, wakiwemo wachezaji wa klabu moja ya soka ya Brazil, imeanguka eneo la Medellin nchini Colombia.
                      Timu hiyo ilipangiwa kucheza mechi ya awamu ya kwanza ya fainali ya Copa Sudamericana

Maafisa wanasema watu sita wamenusurika.
Ndege hiyo inadaiwa kupata hitilafu za mfumo wake wa umeme.

Ndege hiyo ilikuwa safariki kutoka Bolivia na ilikuwa imewabeba wachezaji wa timu ya Chapecoense, ambao walikuwa wamepangiwa kucheza mechi ya fainali ya Copa Sudamericana, dhidi ya timu ya Medellin, Atletico Nacional.

Mechi ya awamu ya kwanza ya kombe hilo, la pili kwa umuhimu Amerika Kusini, ilikuwa imepangiwa kuchezwa Jumatano lakini sasa imesitishwa.

Timu hito inayotoka mji wa Chapeco, kusini mwa Brazil, ilipandishwa kucheza ligi ya daraja ya kwanza nchini Brazil mwaka 2014 na ilifika fainali ya kombe hilo la Sudamericana kwa kulaza San Lorenzo ya Argentina.

Taarifa zinasema ndege hiyo muundo wa British Aerospace 146 ambayo imekuwa ikitumiwa na shirika la ndege la Lamia la Bolivia ilikuwa na abiria 72 na wahudumu tisa.

 
Timu hiyo ilipangiwa kucheza mechi ya awamu ya kwanza ya fainali ya Copa Sudamericana
Ilianguka eneo la milimani nje kidogo mwa mji wa Medellin majira ya (saa mbili asubuhi Afrika Mashariki).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa uwanja wa ndege, marubani walisema ndege hiyo ilikuwa imepata matatizo katika mfumo wake wa umeme.

Meya wa Medellin Mayor Federico Gutierrez amesema ajali hiyo ni "janga kubwa".

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Jose Maria Cordova de Rionegro uliopo Medellin, wamesema juhudi zote zinafanywa kuwaokoa manusura.

Hali mbaya ya hewa inazuia maafisa kufikia eneo la mkasa kwa urahisi.
Hakukutokea moto baada ya ndege hiyo kuanguka, jambo ambalo linaibua matumaini ya kupatikana kwa manusura.

Klabu ya Chapecoense
  • Ilianzishwa 1973.
  • Ikapandishwa kucheza ligi ya daraja ya kwanza Brazilian, Serie A, mara ya kwanza 2014. Imo nambari tisa ligini kwa sasa.
  • Walikuwa wanaelekea kucheza fainali ya Copa Sudamericana, mshindi hufuzu kucheza Copa Libertadores, shindano kubwa la klabu Amerika Kusini.
  • Jiji lao la nyumbani ni Chapeco katika jimbo la Santa Catarina, Brazil
source:BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here