TAFOPA YATOA WITO KWA WADAU NA MASHIRIKA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, November 30

TAFOPA YATOA WITO KWA WADAU NA MASHIRIKA

Na Mustafa Ismail

Watanzania na wadau wakuu wa sekta binafsi wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa wadau wa uendelezaji wa viwanda vya usindikaji utakao fanyika jumamosi ya terehe 3 desemba mwaka huu katika ukumbi wa mwalimu nyerere convention centre jijini Dare es salaam

Akiongea na waandishi wa habari Jijini daresalaam mwenyekiti wa chama cha {Tanzania Food Processors association [TAFOPA]} Suzy Laiser mewataka wadau kujitokeza katika mkutano huo utakao hudhuriwa na washiriki takariban mia moja wakiwemo mawaziri wa wizara mbalimbali, wawakilishi wa mikoa, wakurugunzi wa halamashauri; wakurugenzi wa mashirika ya kimataifa na wadau wa maendeleo sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Laiser amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuzindua uanzishwaji wa uendelezaji wa maeneo ya viwanda vya usindikaji[Food Processing Industrial Parks] kuhamasisha na kutafuta washirika kutoka katika mshirika ya kimataifa serikali na sekta binafsi.

Aidha Laiser aliongeza kuwa mkutano huo utakuwa fursa pekee ya kushughulikia changamoto zinazowakabili wasindikaji wa vyakula nchini “changamoto kubwa ya wasindikaji ni maeneo safi na salama ya kusndikia kwani wengi wanasindikia majumbani hivyo basi wanakabiliwa na changamoto za kukidhi viwango vya kitaifavta ubora na usalama wa chakula”

Naye mtaalamu na mshauri wa chama hicho Gloria Kavishe amesema kuwa chama kina malengo ya kuhakikisha bidhaa zinazotolewa na chama hicho zinasambazwa kote nchini na nje ya nchi “tumalengo yakusambaza bidhaa zetu ndani na nje ya nchi kwani tunatarajia kupata mitambo ya kutosheleza na yenye hadhi ya juu”

Aidha Kavishe aliongeza kuwa mkutano huo unaunga mkono juhudi za Mama Samia Suluhu Hassan za kuendeleza “cottage industry” kama mkakati wa kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Mkutano huo utaongozwa na Makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan aliyeteuliwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa  kuwa mwakilishi wa mashariki na kusini katika mkakati wa kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Chama hicho chenye wanachama zaidi ya 600 kimetoa mafunzo ya usindikaji kwa takriban watu 7000 na kina lenga kutoa mafunzo zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here