WAKAZI WA TEMEKE KUPATWA MAJANGA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, November 28

WAKAZI WA TEMEKE KUPATWA MAJANGA



Na Mustafa Ismail
                       Related image

Wakazi wa wilaya ya temeke mtaa wa sambwisi wamelalamikia miundombinu mibaya ya barabara  katika makutano ya barabara ya sambwisi na chihota ambapo maji hutulia katika barabara hizo kero ambayo wameitaja kurudisha nyuma maendeleo kwani hukwamisha shughuli za uchukuzi na biashara pindi mvua inaponyesha.

Akiongea na Mkwelitz mapema wiki hii mmoja wa wakaazi wa eneo hilo na mfanya biashara Musa Ali ameelekeza kidole cha lawama kwa serikali ya wilaya hiyo na kusema kuwa serikali hiyo inakwepa majukumu “Mimi binafsi naona serikakali ya wilaya ya temeke imeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa mfano ukiangalia katika barabara hii imejaa maji mpaka hatuwezi kufanya biashara” alisema ali

Aidha Ali aliongeza kuwa kero zao wameziwasilisha kwenye serikali ya mtaa huo lakini bado tatizo hilo la muda mrefu halijatatuliwa “Tumekuwa tukipeleka malalamiko yetu mara kwa mara katika serikali ya mtaa wetu lakini lakushangaza hatuoni mabadiliko mpaka tumechoka “ Alisistiza Ali.

Kwa upande wake mmoja wa madereva wanaotumia barabara hiyo Mohammed Bakari ameeleza maskitiko yake juu ya changamototo wanazokumbana nazo kwenye sekta ya uchukuzi hasa msimu wa mvua “Binafsi naskitika sana na hali ya barabara zetu gari zinakwama inatubidi tuzunguke mzunguko mrefu sasa inatupotezea maesabu” alisema Bakari

Mkwelitz BLOG ilifanya juhudi za kumsaka mkuu wa wilaya ya temeke ili kulidadavua suala hilo lakini juhudi zetu hazikufua dafu.

Malalamishi ya wakaazi hao yamekuja siku chache tu baada ya mvua kali iliyoshuhudiwa mapema wiki hii katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake iliyodumu kwa takriban siku nzima na kuleta athari kwa baadhi ya maeneo jijini humo.

Tatizo la miundombinu mibovu hususan  ya barabara limekuwa tatizo sugu nchini huku kidole cha lawama kikitupiwa serikali za wilaya na mikoa kwakulifumbia macho swala hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here