CRISTIANO RONALDO BIGWA WA DUNIA NA MAHREZ BIGWA AFRIKA,HABARI ZOTE HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, December 13

CRISTIANO RONALDO BIGWA WA DUNIA NA MAHREZ BIGWA AFRIKA,HABARI ZOTE HAPA

Cristiano Ronaldo
CRISTIANO RONALDO ameshinda Tuzo maarufu na iliyotukuka ya Ballon d'Or kutoka Listi ya Wagombea 30 akiwemo alieishika kmWaka Jana Lionel Messi.
Hii sasa ni mara ya 4 kwa Ronaldo kutwaa Tuzo hii akizidiwa mara 1 tu na Messi.

Ballon d'Or inasimamiwa na Jarida maarufu France Football na Mshindi wake hupatikana kwa Kura za Wanahabari 173 toka kila pembe ya Dunia.


France Football imekuwa ikisimamia Ballon d'Or kila Mwaka tangu 1956 lakini kwa Miaka 6 iliyopita wamekuwa wakishirikiana na FIFA na Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka kuitwa FIFA Ballon d'Or 
Image result for ronaldo

Lakini Mwezi Septemba FIFA ikajitoa na kuanzisha Tuzo yao ikuwemo zile za Kinamama, Timu ya Mwaka na Washindi wake wanategemewa kutangazwa kwenye Hafla maalum hapo Januari 9 huko Zurich.

Ronaldo, ambae amefunga Bao 48 katika Mechi 52 kwa Klabu yake Real Madrid na Nchi yake Portugal kwa Mwaka huu 2016, hakuwepo huko France kuipokea Tuzo hiyo kwa vile yuko Japan na Real ambao watashiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.

Mwaka huu, Ronaldo aliisaidia Real kutwaa Ubingwa wa Ulaya na pia Portugal kubeba EURO 2016, Kombe la Mataifa ya Ulaya.

Ronaldo, ambae pia ametwaa Ballon d'Or katika Miaka ya 2008, 2013 na 2014, ameeleza: “Kwangu mimi hii ni heshima kubwa kutwaa huu Mpira wa Dhahabu kwa mara ya 4. Ni ndoto iliyotimia. Nimefurahi sana! Nawashukuru Wachezaji wenzangu, toka Timu ya Taifa na Real Madrid. Basikia fahari na furaha kubwa!”

RONALDO katika Namba:
4 – Ushindi Ballon d'Or Miaka ya 2008, 2013, 2014 na 2016 akiteuliwa mara 8 kugombea.
137 – Mechi kwa Portugal.
68 – Goli kwa Portugal.
4 – Mwaka huu amekuwa Mchezaji wa Kwanza kufunga katika Fainali za EURO (2004, 2008, 2012 na 2016).
80 – Pauni Milioni walizolipa Real Madrid kumnunua kutoka Manchester United 2009.
17 – Rekodi ya Bao nyingi kwa Msimu Mmoja wa UEFA CHAMPIONZ LIGI (2014).
270 – Idadi ya Magoli kwa Real Madrid katika Mechi 248 za La Liga.
9 – Jumla ya Mabao kwenye EURO akifungana na Michel Platini kuwa Wafungaji Bora wa Mashindano hayo ya Mataifa ya Ulaya.
14.1 – Pauni anazovuna kutoka kwa Udhamini wa Nike.
48,756,584 – Wafuasi Mtandao wa Twitter.
118,164,346 – Wafuasi Mtandao wa Facebook


KWA UPANDE WAKE RIYAD MAHREZ AMEJINYAKULIA TUZO YA MWANASOKA WA AFRIKA KWA MUJIBU WA BBC

 Riyad Mahrez baada ya kupokea tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2016
Riyad Mahrez ametawazwa kuwa Mwanakandanda Bora wa Afrika wa BBC wa Mwaka 2016.

Mashabiki kutoka kila pembe ya dunia walimpigia kura nyingi kiungo huyu wa kati wa Algeria na Leicester kuliko Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Sadio Mane na Yaya Toure.

Mahrez ameambia BBC Sport: "Naam, [tuzo hii] ina maana kubwa sana kwa sababu bila shaka mimi ni Mwafrika na ni jambo kuu sana kwa mchezaji wa Afrika nafikiri, kwa hivyo nina furaha isiyo na kifani, najivunia kuipokea.."
Tuzo hii ni kilele kwenye mwaka mzuri kwa mchezaji huyu wa miaka 25, ambaye tayari amejishindia taji la Ligi ya Premia na alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la Wachezaji Uingereza.

Mahrez ametambuliwa kwa uchezaji wake mzuri kama mchawi katika wingi, ambaye familia yake inatoka kijiji kidogo kwa jina El Khemis nchini Algeria, ambaye alitikisa Ligi ya Premia.

Alisaidia sana Leicester City kushinda ligi bila kutarajiwa, ambapo alifunga mabao 17 na kusaidia ufungaji wa mabao 11 kuwawezesha kushinda, licha ya uwezekano wao kushinda mwanzoni mwa msimu kuwa 5000-1 pekee.

Mwezi Mei, Mahrez aliibuka Mwafrika wa kwanza kuteuliwa mchezaji bora zaidi ligini na wachezaji wenzake, miaka miwili tu baada yake kujiunga na Leicester kutoka Le Havre kwa £400,000.
Ni ufanisi mkubwa kwa mchezaji huyu aliyeanza maisha akicheza soka katika barabara za mtaa alipokuwa mtoto ambaye sasa amekuwa nyota anayeshindana na wachezaji bora zaidi duniani katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Amefunga mabao manne katika mechi tano alizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, ishara kwamba anaweza kutamba hati katika ligi zenye ushindani mkubwa zaidi.
Amefana pia akicheza soka ya kimataifa.
Katika mechi tano alizochezea Algeria, amefunga mabao mawili na kusaidia ufungaji wa magoli matano, na akawezesha Mbweha hao wa Jangwani kufuzu kwa mfainali za Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwezi ujao. 

Kadhalika, ufanisi wake umetambuliwa na shirikisho la soka duniani FIFA, ambao walimuorodhesha kwenye orodha ya wachezaji watakaoshindania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani - Mwafrika pekee katika orodha ya wachezaji 23.

Mahrez sasa anajiunga na vigogo wa soka Afrika , wakiwemo Abedi Pele, Jay-Jay Okocha na Didier Drogba, ambao wamewahi kushinda Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka.
Na ikizingatiwa kwamba bado ana miaka mingi ya kucheza, bado kuna muda kwake Mahrez kuwafurahisha mashabiki, ambao wameonesha jinsi wanavyompenda.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here