MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA,MBEYA,IRINGA NA NJOMBE ZAONGOZA TANZANIA,HABARI ZOTE HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, December 29

MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YASHUKA,MBEYA,IRINGA NA NJOMBE ZAONGOZA TANZANIA,HABARI ZOTE HAPA

Image result for Dkt. Leonard Maboko
Kutokana na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kupungua kwa asilimia 50 duniani kote na kupelekea watu milioni 2.1 tu kuambukizwa Virusi vya Ukimwi katika mwaka 2015,kumeibua matumaini mapya ya kuwa na watu wasio na maambukizi ya virusi vya Ukimwi ifikapo mwaka 2030.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko aliwaambia waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam kuwa, nchini Tanzania maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi nayo yameshuka kwa asilimia 20 ambapo watu 54,000 wameambukizwa virusi hivyo kwa mwaka 2015 pekee.

Dkt. Maboko alisema, Ukimwi bado ni janga kubwa duniani na taifa kwa ujumla huku akitaja kundi la wanawake kuwa ndilo lina kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU huku mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya ukiwa na kiwango cha juu cha maambukizi hayo kitaifa.

Aidha, alisema serikali imejiwekea mikakati kuhakikisha kuwa waliogundulika kuwa wameathirika wanaanzishiwa dawa, kuhimiza matumizi ya mpira wa kiume, kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 29 na kutoa elimu kwa wanawake wanaojihusisha na ngono, kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here