MH PAUL MAKONDA KESHO KUKUTANA NA MACHINGA,HABARI KAMILI HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, December 14

MH PAUL MAKONDA KESHO KUKUTANA NA MACHINGA,HABARI KAMILI HAPA

Image result for MAKONDA
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kesho anatarajia kukutana na wafanyabiashara ndogo maarufu machinga ili kujua sababu ya kutokuwa tayari kwenda katika maeneo waliyopangiwa.
Makonda alisema lengo la kukutana na wafanyabiashara hao ni kujua kwa nini hawapo tayari kwenda katika maeneo waliyotengewa na kuangalia namna bora ya wao kufanya biashara zao ili kuondoa usumbufu uliopo sasa.
“Nitakutana na wamachinga katika mkoa wangu, nikiambatana na Wakuu wa Wilaya ili niweze kujua ni kitu gani kinachowafanya wao kushindwa kwenda katika maeneo yaliyotengwa. ”
Aidha, Makonda alisema hawezi kuruhusu utaratibu unaofanywa na machinga hao, ambao baada ya kauli ya rais wamerejea na kuweka biashara zao hata sehemu za watembea kwa miguu na kusababisha kero.
“Siwezi kuruhusu utaratibu uliopo sasa, wamefikia hatua ya kuziba barabara hata magari yanashindwa kupita wananchi wanapata taabu, nitakwenda kuonana nao na nitawasikiliza na baada ya kuwasikiliza tutakuja na uamuzi,” aliongeza Makonda.
Juzi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ilisema inajiandaa kuanzisha Sabasaba Bonanza ili watu wasio na maeneo ya kufanya biashara, wakiwemo machinga, kutumia Viwanja vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu J. K Nyerere maarufu Sabasaba, kufanya biashara zao.
Kaimu Mkurugenzi wa Tan- Trade, Edwin Rutageruka alisema TanTrade itaanzisha bonanza angalau mara moja kwa wiki, lakini kabla ya kufanya hivyo, watafanya utafiti wa kuanzisha Sabasaba bonanza ili watu ambao hawana maeneo ya kufanyia biashara wakauze bidhaa zao katika eneo hilo.
Hivi karibuni Rais Magufuli alimuagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kusitisha mara moja utekelezaji wa kazi ya kuwaondoa machinga katika Jiji la Mwanza pamoja na mikoa mingine mpaka hapo mamlaka husika zitakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha machinga wenyewe.
Baada ya kauli hiyo ya rais, wafanyabiashara wengi walianza kurejea katika maeneo ya katikati ya miji, jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wananchi hasa watembea kwa miguu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here