DROO
ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, itafanyika Leo huko
Nyon, Uswisi na Mabingwa Watetezi Real Madrid ni miongoni mwa Mabingwa 7 ambao
wamo kwenye Vyungu Viwili vya Timu Nane Nane ambazo zitapambanishwa.
Timu Moja ya Chungu A, ambacho ni cha Washindi wa Makundi,
itapambanishwa na nyingine toka Chungu B, ambacho ni Timu zilizomaliza Nafasi
za Pili.
Kanuni itakayosimamia Droo hii ni kuwa Timu toka Kundi Moja
hazitakutanishwa na pia Timu toka Nchi moja hazitapambanishwa.
CHUNGU A:
Arsenal (Kundi A, England), Napoli (B, Italy), Barcelona (C,
Spain), Atlético Madrid (D, Spain), Monaco (E, France), Borussia Dortmund (F,
Germany), Leicester City (G, England), Juventus (H, Italy)
CHUNGU B:
Paris Saint-Germain (A, France), Benfica (B, Portugal), Manchester
City (C, England), Bayern München (D, Germany), Bayer Leverkusen (E, Germany),
Real Madrid (F, Spain), Porto (G, Portugal), Sevilla (H, Spain)
Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL zitachezwa Tarehe
14/15 na 21/22 Februari na Marudiano ni Tarehe 7/8 na 14/15 Machi.
Lakini mbali na hapo tena upande wa EUROPA LEAGUE
LEO
huko Lyon, uswisi itafanyika Droo yakupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu
32 ya UEFA EUROPA LIGI hapo Jumatatu Desemba 12.
Timu 24 zilizofuzu Makundi ya Mashindano haya na 8 zilizotoka UEFA
CHAMPIONZ LIGI na kuletwa EUROPA LIGI baada ya kumaliza Nafasi ya 3 kwenye
Makundi yao zitawekwa katika Droo hiyo.
Timu hizo zimewekwa kwenye Vyungu Viwili ambapo Timu toka Chungu
Namba 1 itapambanishwa na Timu toka Chungu Namba 2.
Kanuni ambazo zitatawala Droo hiyo ni kuwa Timu zilizokuwa Kundi
Moja au toka Nchi moja hazitakutanishwa.
Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zitachezwa
Alhamisi Februari 16 na Marudiano ni Februari 23.
CHUNGU NAMBA 2: Anderlecht (BEL), Astra Giurgiu (ROU), Athletic Club (ESP), AZ Alkmaar (NED), Borussia Mönchengladbach* (GER), Celta Vigo (ESP), Gent (BEL), Hapoel Beer-Sheva (ISR), Krasnodar (RUS), Legia Warszawa (POL)*, Ludogorets Razgrad (BUL)*, Manchester United (ENG), Olympiacos (GRE), PAOK (GRE), Rostov (RUS)*, Villarreal (ESP)
*Timu zilizotoka UEFA CHAMPIONZ LIGI
No comments:
Post a Comment