KLABU ya Real Madrid imepangwa
kucheza na Sevilla katika hatua ya timu 16 bora ya michuano ya Kombe la Mfalme.
Mabingwa hao wa Ulaya na Dunia
wanatarajiwa kuchuana na Sevilla iliyo chini ya Jorge Sampaoli ambao
wanashikilia nafasi ya tatu katika La Liga, ikiwa kama marudiano baada ya
kukutana katika Super Cup ya UEFA Agosti mwaka huu ambapo Madrid waliibuka
kidedea.
Ratiba hiyo inamaanisha Madrid na
Sevilla watakutana katika mechi tatu katika kipindi kisichozidi siku 11 mwezi
ujao, kufuatia mchezo wa ligi baina yao kuwa Januari 15.
Mabingwa watetezi wa taji hilo
Barcelona wao watakwaana na Athletic Bilbao ambao waliwafunga katika fainali ya
msimu uliopita, wakati Atletico Madrid wao watapambana na Las Palmas.
Valencia wao watapambana na Celta
Vigo, Villarreal watacheza na Real Sociedad, Osasuna dhidi ya Eibar na
Deportivo La Coruna watachuana na Alaves.
Mechi za mkondo wa kwanza
zinatarajiwa kuchezwa Januari 4 huku zile za marudiano zikichezwa Januari 11.
No comments:
Post a Comment